MAKONDA ATANGAZA AJIRA KWA JKT, MGAMBO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na waandishi wa habari alipotangaza JKT na mgambo kufika ofisini kwake kupatiwa ajira ya kusimamia usafi na kuwatoza faini wachafuzi wa mazingira jijini. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mgambo ambao hawana kazi kufika ofisini kwake Ijumaa ya Julai 06 mwaka huu ili kupatiwa ajira ya kusimamia usafi na kuwatoza faini wachafuzi wa mazingira katika jiji la Dar es Salaam. Makonda amesema katika fedha itakayotozwa kwa wachafuzi wa mazingira asilimia 50% itakwenda kwenye halmashauri na asilimia 50% kwa vijana wa JKT na mgambo ambapo kabla vijana hao hawajakabidhiwa jukumu hilo watapewa mafunzo ya sheria ya usafi. “Katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana sambamba na kuufanya mji kuwa katika hali ya usafi baada ya mbinu nyingi zilizokuwa zikitumiwa kuhamasisha usafi kutokuwa na matokeo maz...