Wanafunzi wanne kati ya watano wa Shule ya Msingi Ndolage, Kata ya Kamachumu, Kagera wamekamatwa wakidaiwa kutoroka shule na kwenda kutafuta kazi za ndani mjini Bukoba. Wanafunzi hao wenye miaka 11 hadi 14 walitoroka Aprili 25 wakiwa na sare za shule. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ndolage, Frederick Byarugaba alisema wanafunzi hao (majina tunayahifadhi) walitoka nyumbani kwao Kitongoji cha Buganda B, Kamachumu na walipata usafiri wa kuelekea Bukoba Mjini. “Baada ya taarifa hizo kusambaa kuwa wanafunzi wametoroka, uongozi wa shule ulitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, Kituo cha Kamachumu, Muleba,” alisema Byarugaba. Alisema watoto hao walionekana kwa mara ya kwanza, Manispaa ya Bukoba wakitembea pamoja na baadhi ya watu wakiwamo abiria waliwakamata na kutoa taarifa polisi na kwa uongozi wa shule. “Walikuwa na utoro wa rejareja na mara kadhaa wamekuwa wakikanywa kuhusu tabia mbaya ya utoro, hivyo baada ya wazazi kutoa taarifa ya kutoonekana nyumbani tulianza kusamb...