MAAFA YA MV BUKOBA KILA KIFO NA SIKU YAKE May 21 kila mwaka tunakumbuka maafa ya MV BUKOBA 😿 Kila binadamu atakufa, lakini kila kifo kina siku yake. Nyaisa Simango, katika makala haya ana tudhihirishia hivyo. Vinginevyo ni vipi mtu anaweza kuelezea alivyo nusurika wakati mamia ya wenzake walio kuwa katika meli moja walishindwa kujiokoa. Ilikuwa sio siku yake. Ziwa victoria limekuwepo kwa karne na karne, watu wanaoishi kuzunguka ziwa hilo wamekuwa wakijishughulisha na shughuli mbalimbali. Kuvumbuliwa kwa Ngalawa, Jahazi, Boti, na meli kumewezesha kazi za usafirishaji kuwa rahisi. Bila shaka Simango alipo itwa na mkuu wake wakazi na kuarifiwa kuwa itabidi aende Bukoba kumpeleka mfungwa kusikiliza rufaa ya kesi yake alifurahi kwani angeweza kuona mandhari nzuri njiani. Ijapokuwa yeye anatoka katika nmkoa unao pakana na ziwa bado angefurahia kula samaki. Nakwavile hakuwahi kufika bukoba, safari ingempa fursa nzuri ya kutalii mjini...