TANGA RAHA SEHEMU YA 45

AGE………………18+ WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA ILIPOISHIA Nikabaki nikiwa nipo kimya, kama nimemwagiwa maji ya baridi, swali la kwanza kujiuliza kichwani ni mbinu gani waliyo itumi hadi mimi leo nipo hai.Nikiwa ninaendelea kuliwazia ninalo liwaza nikamuona Olvia Hitler akiwa amesimama nyuma ya Rahma huku macho yake yakimwagikwa na machozi ya damu ENDELEA Nikabaki nikiwa nimeduwaa, pasipo kuzungumza kitu chochote, Olvie akaanza kutingisha kichwa taratibu huku machozi ya damu yakiendelea kumwagika kwa wingi, akauinua mkono wake mmoja na kuanza kuniita taratibu, hapa ndipo nilipoiona mkono wake ukiwa umejaa damu nyingi. “Walipo niambia kwamba umekufa, ikanilazimu kufanya kitu ambacho kingeurudisha uhai wako, kutokana sikuhitaji uweze kupotea kiurahisi maishani mwangu, wakati bado sijaisha nawe vya kutosha” Hata Rahma alicho kizungumza sikukitilia maanani kwa maani macho, na akili yangu zote zilikuwa zipo kwa Olvia aliye simama nyuma ya mke wangu Rahma.Olvia Hitler akaunyan...