Baadhi ya wagonjwa wakiandaliwa kwa safari ya Bugando Mwanza eneo la Uwanja wa ndege Ruganzo,wilayani Ngara mkoani Kagera.
|
Afisa mwandamizi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wilayani Ngara Bi. Irene Babu.
Idadi ya vifo vya Wakimbizi waliopata ajali kwenye mteremko wenye kona kali wa K9 katika kijiji Kasharazi wilayani Ngara mkoani Kagera, imeongezeka na kufikia 8 baada ya wawili kufariki wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Murugwanza na mmoja katika hospitali ya Nyamiaga.
|
Majeruhi wote waliopata rufaa wamekwishasafirishwa kwa ndege ya UNHCR kwenda hospitali ya Bugando kupitia uwanja wa ndege wa Ruganzo uliopo wilayani Ngara
|
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Murugwanza ya Wilayani NgaraDr. Remmy Andrew amesema katika Hospitali hiyo alipokea Majeruhi 65 kati yao 30 ni Wanawake na 35 ni Wanaume na kwamba waliotibiwa na kuruhusiwa ni 40 na waliopatiwa rufaa kwenda Hospitali ya Bugando ni 7
Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Nyamiaga Dr. Simon Kyamwenge amesema Hospitali hiyo ilipokea Majeruhi 31 kati yao Wanaume ni 24 na Wanawake 7 na kwamba mpaka sasa ameruhusiwa mtu mmoja pekee.
Pia Dr. Kyamwenge amesema Majeruhi 12 wenye hali mbaya wamepewa rufaa ya kupelekwa katika Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
|