MCHELE WA PLASTIKI’ BALAA UPYA!
Magunia ya mchele. KWA siku kadhaa sasa tangu kuibuka kwa taharuki nchini juu ya uwepo wa mchele wa bandia almaarufu mchele wa plastiki huku mamlaka za serikali zikikanusha ishu hiyo, lakini kadiri siku zinavyosonga, jambo hilo limekuwa likiibua balaa upya. Mapema wiki hii, mwanamke mmoja aliyejukana kwa jina la Zuwena Mapunda, mkazi wa Kimara-Baruti jijini Dar alizua timbwili zito na la aina yake baada ya kudai kuuziwa mchele unaodaiwa kuwa ni wa plastiki. Zuwena aliuziwa mchele huo na mfanyabishara aliyetajwa kwa jina moja la Kijagwa. Akizungumza na Amani mbele ya duka la nafaka la Kijagwa lililopo Kimara-Baruti, Dar huku kukiwa na umati uliotaka kuushuhudia mchele huo baada ya kuwepo kwa madai hayo kwa muda mrefu, Zuwena alisema kuwa, alinunua mchele huo kwenye duka hilo kwa ajili ya chakula cha familia. Zuwena alisema kuwa, baada ya kuupika kwa muda mrefu bila kuiva ndipo alipouchunguza kwa kuufinyanga na kuudunda chini ambapo alishangaa kuona unadund...