SIMBA WAIPIGIA MAGOTI AZAM FC KWA MANULA


Kipa wa Azam FC, Aishi Manula.
 UONGOZI wa Klabu ya Simba, umeipigia magoti Azam FC imruhusu Aishi Manulaaweze kushiriki mazoezi na klabu hiyo mapema kwa kuwa bado ana mkataba wa mwezi mmoja na timu hiyo.
Inadaiwa kuwa Manula ameshamalizana na Simba kwa mkataba wa miaka miwili lakini hataweza kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa timu hiyo kwa kuwa bado mkataba wake na Azam FC haujamalizika.
Taarifa ambazo MASHELE BLOG imezipata ni kuwa uongozi wa Simba umeiomba Azam FC kumruhusu Manula mapema ili akafanye mazoezi na kikosi hicho kilichopoAfrika Kusini ili kuepuka kesi kama ilivyokuwa kwa Hassan Kessyalivyokwenda Yanga.
Ulipotafutwa uongozi wa Azam FCkuzungumzia suala hilo ulisema kwa upande wao wanatambua kuwa Manula ni mchezaji wao hadi pale atakapomaliza mkataba na si vinginevyo.
“Manula bado ni mchezaji wetu hadi atakapomaliza mkataba wake, pia yeye mwenyewe ndiye anatakiwa aseme kama amemaliza mkataba ama la, lakini taarifa za Simba kufanya mazungumzo bado hazijanifikia,” alisema Mwenyekiti waAzam FC, Idrisa Nassor  jiunge na masshele blog kwa kufollow on instagram tafuta massheleblog, pia jiunge na blog hii watsapp kwakutext wasap +255766605392 andika masshele sport 

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?