Umeiona simba mpya? Hadi raha
STRAIKA Mghana, Nicholas Gyan, kutoka Ebusua Dwarfs, amekamilisha orodha ya nyota wapya waliosajiliwa ndani ya Simba kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano.
Mabosi wa timu hiyo wameweka bayana kikosi chao kipya cha Wekundu wa Msimbazi ambacho kwa sasa kipo Afrika Kusini kikijiandaa na msimu huo mpya ambapo Simba itacheza Ligi Kuu Bara na Kombe la Shiriisho Afrika.
Mghana huyo aliyetupia kambani mabao 11 katika Ligi Kuu Ghana, ndiye mchezaji anayetajwa kukamilisha idadi ya waliosajiliwa Msimbazi kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe.
Hanspoppe aliwataja nyota wengine 11 ambao dili zao zimekamilika huku akidai kwamba bado hawapo katika nafasi nzuri ya kumtangaza kipa, Aish Manula, kuwa ni mchezaji wao halali.
Bosi huyo aliwataja wachezaji ambao tayari mambo yao yamekamilika kuwa ni makipa Said Mohammed ‘Nduda’ na Emmanuel Mseja, mabeki Yusuf Mlipili, Salim Mbonde, Erasto Nyoni, Ally Shomary, Jamal Mwambeleko na Shomary Kapombe.
Bilionea huyo aliwataja wengine ni washambuliaji Emmanuel Okwi, John Bocco na Gyan ambaye anajiunga moja kwa moja na kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Afrika Kusini baada ya uhamisho wake kutoka Ebusua Dwarfs ya nchini Ghana kukamilika.
“Kuhusu Haruna Niyonzima na Aishi Manula bado tupo nao katika mazungumzo,” alisema Poppe ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba kwa miaka mitano sasa.
Hata hivyo Masshele blog linafahamu kwamba Niyonzima na Manula tayari wamesaini mikataba ya miaka miwili Msimbazi ila mabosi hao wameamua kuacha kuwaweka hadharani kutokana na sababu mbalimbali.
Manula bado mkataba wake na Azam haujamalizika hivyo Simba inagopa kuingia kwenye mtego uliowakuta Yanga msimu uliopita ambapo walimsaini beki Hassan Kessy kabla ya siku ya mwisho ya mkataba wake na kupigwa faini ya Sh 53 milioni.
Kwa upande wa Niyonzima, Simba imepanga kuendelea kuufanya usajili wake siri licha ya kwamba mkataba wake na Yanga tayari umekwisha. Kwa mujibu wa mmoja wa vigogo wa Simba ni kwamba wamepanga kumtambulisha staa huyo wakati maalumu ili kuwaumiza zaidi Yanga waliomuacha kishingo upande.
WALIOTEMWA
Kamati ya Poppe ilithibitisha timu hiyo imeachana na wachezaji; Hija Ugando, Frederic Blagnon, Novaty Lufunga, Hamad Juma, Janvier Bokungu, Dennis Richard na Ibrahim Ajibu ambaye tayari amesaini Yanga.
Wengine ni Pastory Athanas aliyepelekwa Singida United kwa mkopo na kipa Manyika Peter Jr anayepelekwa Mtibwa kwa mkopo pia. Wengine ambao Poppe hakuwataja lakini wanaachwa ni kipa Mghana, Daniel Agyei.
Zali limemwangukia winga, Jamal Mnyate, aliyeongezewa mkataba wa mwaka mmoja na Juma Liuzio aliyegoma kwenda Sauzi akitaka mkataba
Comments
Post a Comment