UNOMINISHAJI
By IkS UDSM UNOMINISHAJI NOMINO ZALIKA/UNOMINISHAJI Unominishaji kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2007) wanasema ni hali ya kuunda nomino kutoka katika kategoria nyingine ya neno. Kategoria hizi zaweza kuwa kitenzi, kivumishi au hata nomino yenyewe. Ø Kwa hiyo vinominishi (o, i) vinaweza kunominisha vitenzi vya Kiswahili katika mazingira yafuatayo: Tukianza na kinominishi (o); kinominishi “o” huweza kunominisha vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati “a”. Kwa mfano: tenda→ tend-o Andika → andik-o Piga → pig-o Pata → pat-o Jenga → jeng-o Fundisha → fundish-o Ona → on-o Pamba → pamb-o Ø Hata hivyo kuna baadhi ya vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati “a”ambavyo havinominishwi na kinominishi “o” mfano wa vitenzi hivyo ni kama lowa, tembea nk. Ø Pia kinominishi “o” huweza kunominisha vitenzi kwa kuambatana na vinyambulishi (-i-) au (-li-) ka...