KAZI YA INI (funtion of liver)

KAZI YA INI MWILINI INI: Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. Ni kiungo ambacho kinahitaji kulindwa na kukingwa pamoja na kusafishwa mara kwa mara. KAZI YA INI MWILINI 1. Ini lina kazi ya uchujaji wa sumu, inachuja sumu kwenye damu ambayo huingia kwa njia ya vyakula, vinywaji (bila kusahau vinywaji vikali), hewa tunayovuta, sigara, pamoja na dawa tunazotumia. 2. Vile vile, hutoa nyongo ambayo kazi yake kubwa ni kusaga mafuta na protini kutoka kwenye chakula tulacho. 3. Pia, ini hukibadilisha chakula na kufanya tupate nguvu mwilini. Hivyo basi, tunahitaji kulilinda ini ili liweze kufanya kazi yake ya uondaji wa sumu na kusaga mafuta na protini kama ilivyokusudiwa. Mara nyingi imeonekana kwa mtu mwenye shida ya ini kuwa akijisikia uchovu mara kwa mara hata kama hajafanya kazi za kuchosha. Hii tutokea kwa kuwa ini limezidiwa na haliwezi kufanya kazi yake ya kuhakikisha mwili unapata nguvu. VYAKULA VINAVYOLINDA NA KUSAFISHA INI 1. Kitunguu saumu: Inasaidia ini kutoa...