Posts

RC Kilimanjaro Anna Mghwira akutwa na maambukizi ya corona

Image
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Anna Mghwira ametangaza kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo siku tatu zilizopita. "Kazi yangu inahusiana na muingiliano wa watu ndipo nikaamua  kupima na majibu yamekuja na yameonyesha kuwa ninamaambukizi ya virusi vya corona mimi mwenyewe sionyeshi dalili za ugonjwa sijisikii homa, sikohoi wala sisikii dalili yoyote ila vipimo vimekuja hivyo kwahiyo hii inaonyesha watu wengi wanatembea wakijijua kuwa wapo salama kumbe hawapo salama" alisema RC Mghwira

Watu 150 wafariki kwa ugonjwa usiojulikana nchini Nigeria

Image
Watu  150 waripotiwa kufariki katika jimbo la Kano  kwa maradhi yasiojulikana nchini Nigeria. Mkurugenzi wa hospitali ya mafunzo ya udaktari  Aminu Kano,  Isa Abubakar   amefahamisha kuwa watu  150 wamekwishafariki  kwa maradhi ambayo hayajajulikana  nchini humo. Mkurugenzi huyo amesema kwamba vifo hivyo vimetokea kati ya Ijumaa na Jumapili wiki iliopita. Daktari Isa Abubakar amefahamisha kuwa watu waliofariki ni watu wenye umri wa kuanzia miaka  60. Daktari huyo amewaambia wanahabari kuwa  huenda watu hao wamefariki  kwa virusi vua corona kwa kuwa sio jambo la kawaida idadi kubwa ya watu kufariki kwa mkupuo. Nchini Nigeria ni watu  22 ndio  wamekwishafariki kwa virusi vya corona na wengine  665 wakiwa wamekwishaathirika na virusi hivyo.

Jinsi ya kumjua msichana ambaye hakupendi

Image
Je, unataka kujua msichana havutiwi nawe? Kuna dalili unahitaji kujua ili kuepuka uchungu wa kukataliwa baadaye 1. Anakataa kukupa namba mara ya kwanza? Ikiwa msichana hataki kukupa namba yake ya simu unapomuomba mara ya kwanza, jua ya kwamba hakutaki. Ikiwa atakupa, itachukua muda kufanya hivyo, jua kuwa hataki mambo yako, hivyo ni bora kukoma mapema kwa sababu mtasumbuana bure tu.  2. Amekupa namba isiyo yake?  Msichana akifanya hivi huhitaji kungoja sana kujua kuwa hapendezwi nawe. Kushinda ukimfuata itakuumiza bure tu kwani simu zako zitakuwa zikichuliwa na mtu mwingine. Huenda akalaumu mfumo mbaya ya mawasiliano.  3.Hachukui simu unapompigia?  Unangoja nini kujua hakutaki? Ikiwa msichana atachukua simu mara moja unapopiga, jua ya kuwa anakupenda na ni ishara kuwa mtakuwa marafiki. Lakini akichukua muda kujibu, kimbia 4. Hakutembelei? Ikiwa hatembei kwako, basi ni ishara kwamba hataki kukuona. Hakuna haja ya kumfuatafuata. 5....

Ununuzi wa Tiketi Kufanyika Kwa Njia ya Mtandao ili Kukabiliana na Corona

Image
Katika  kukabiliana na mambukizi ya virusi vya Corona katika vituo vya mabasi serikali imesema mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya mtandao utaanza hivi karibuni kwa mabasi yote yanayofanya safari zake mikoani.   Mbali na mabasi hayo, daladala pamoja na mabasi ya mwendokasi yanatarajiwa (Data center) ambapo mfumo huo utarahisisha huduma na kuondoa adha ya wapiga debe vituoni.   Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandishi Isack Kamwele, wakati wa ukaguzi wa mifumo hiyo jana Dar es Salaam alisema hatua hiyo itafikiwa hivi karibuni ambapo kiu ya serikali ni kuona wananchi wananufaika kwa kuondoshewa adha ya usafiri.   Mhandisi Kamwelwe alisema serikali imefikia hatua ya mwisho ya kuanza kutumika kwa mfumo huo ambapo wananchi watatumia simu kukata tiketi za mabasi na hawatolazimika kutembelea vituoni jambo litakalowaepusha na wizi unaofanywa kupitia ulanguzi wa tiketi na wapiga debe.   “Nimeridh...

Department of kiswahili, Nairobi University

Image
KISWAHILI LINGUISTICS This thematic area includes subsections like phonetics, Kiswahili phonology, Kiswahili ,morphology, Kiswahili syntax, Kiswahili semantics, Kiswahili pragmatics, Discourse Analysis, Historical and comparative studies in Kiswahili, Kiswahili psycho-linguistics and Kiswahili translation and interpretation. The focus of this thematic area is largely to offer Kiswahili description and analysis of Kiswahili language data. This description has to be related to theoretical positions in linguistics. Programmes in this thematic area are offered to undergraduate and postgraduate students. Head  of Thematic Area Dr George Mweri Members of Thematic Area 1)  Prof. Mohamed H. Abdulaziz 2)  Prof. Hamu Habwe 3)  Dr. Iribe Mwangi 4)  Dr. Ayub Mukhwana 5)  Mr. B.G. Mungania 6)  Dr. Prisca Jerono 7)  Ms. Hannah Mwaliwa 8)  Ms  Margaret  Njuguna Degree Programmes/Course Units Link...

VIDEO | Aslay – Mchepuko

Image

CORONAVIRUS: FAHAMU KINACHOTOKEA NDANI YA MWILI MTU AKIPATA VIRUSI HIVI

Image
Coronavirus ilitokea Desemba mwaka jana lakini tayari dunia nzima inakabiliana na janga hili la - Covid-19. Kwa wengi ugonjwa huu unajitokeza nguvu yake ikiwa ya wastani tu lakini baadhi ya watu hufa. Lakini je virusi hivi vinaathiri vipi wili, kwanini baadhi ya watu wanakufa na je tiba yake ikoje? Muda wa  kuatamia wa kirusi cha Corona Hiki ni kipindi ambacho kirusi kinajiimarisha kwenye mwili. Kirusi huingia kwenye seli zinazotengeneza mwili na kuziteka nyara. Coronavirus, inayojulikana pia kama Sars-CoV-2, inaweza kuvamia kwenye mwili unapopumua yaani baada ya mtu mwenye virusi kukohoa ama kushika sehemu yenye virusi hivyo na kushika uso wako. Kwanza inaambukiza seli za kwenye koo lako, njia za kupumua na kwenye mapafu na kuzibadilisha kuwa sehemu ya utengenezaji wa virusi vya corona, na kuzalisha virusi vingi vipya ambavyo vinaenda kuathiri seli nyingi zaidi. Katika hatua hii, bado utakuwa hujaanza kuumwa na kuna baadhi ya watu ambao hata hawaoneshi dali...