Watu 150 wafariki kwa ugonjwa usiojulikana nchini Nigeria


Watu  150 waripotiwa kufariki katika jimbo la Kano  kwa maradhi yasiojulikana nchini Nigeria.

Mkurugenzi wa hospitali ya mafunzo ya udaktari  Aminu Kano,  Isa Abubakar   amefahamisha kuwa watu  150 wamekwishafariki  kwa maradhi ambayo hayajajulikana  nchini humo.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba vifo hivyo vimetokea kati ya Ijumaa na Jumapili wiki iliopita.

Daktari Isa Abubakar amefahamisha kuwa watu waliofariki ni watu wenye umri wa kuanzia miaka  60.

Daktari huyo amewaambia wanahabari kuwa  huenda watu hao wamefariki  kwa virusi vua corona kwa kuwa sio jambo la kawaida idadi kubwa ya watu kufariki kwa mkupuo.

Nchini Nigeria ni watu  22 ndio  wamekwishafariki kwa virusi vya corona na wengine  665 wakiwa wamekwishaathirika na virusi hivyo.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?