Ili mtu aseme ana tatizo hili ni pale anapokosa period au anapata mzunguko usioeleweka baada kipindi cha miezi 6 tokea aache kutumia dawa za uzazi wa mpango. Kwa kitaalamu hali hii inaitwa post pill amenorrhea. Tafiti zinaonesha kuwa kati ya wanawake wanaotumia dawa za uzazi wa mpango aslimia 2 hadi 3% wanapata hali hii. TATIZO HILI HUTOKEAJE. hii inatokana na kuathiriwa kwa utendaji kwazi wa tezi ya pituitari na dawa za uzazi wa mpango. Katika mzunguko wa kawaida tezi ya pituitari huzalisha hormone chochezi ya mayai (follicle stimulating hormone) na hormone ya lutea (lutenizing hormone) ambazo hizi zinachochea kupevuka kwa mayai kwenye mfuko wa mayai (ovari). Mayai yaliyokomaa huzalisha hormone ya estrogen. Pia hormone ya progesterone huzalishwa baada ya yai lililopevuka kuachiliwa kutoka kwenye ovari. Kazi ya hormone hizi ni kuandaa mji wa mimba kulokea yai likirutubishwa na kutunza ujauzito. Kusipokuwa na kurutubishwa kwa yai ule ut...