Ili mtu aseme ana tatizo hili ni pale anapokosa period au anapata mzunguko usioeleweka baada kipindi cha miezi 6 tokea aache kutumia dawa za uzazi wa mpango.
Kwa kitaalamu hali hii inaitwa post pill amenorrhea.

Tafiti zinaonesha kuwa kati ya wanawake wanaotumia dawa za uzazi wa mpango aslimia 2 hadi 3% wanapata hali hii.

TATIZO HILI HUTOKEAJE.
hii inatokana na kuathiriwa kwa utendaji kwazi wa tezi ya pituitari na dawa za uzazi wa mpango.

Katika mzunguko wa kawaida tezi ya pituitari huzalisha hormone chochezi ya mayai (follicle stimulating hormone) na hormone ya lutea (lutenizing hormone) ambazo hizi zinachochea kupevuka kwa mayai kwenye mfuko wa mayai (ovari).

 Tokeo la picha la mfumo wa pituitari
Mayai yaliyokomaa huzalisha hormone ya estrogen. Pia hormone ya progesterone  huzalishwa baada ya yai lililopevuka kuachiliwa kutoka kwenye ovari. Kazi ya hormone hizi ni kuandaa mji wa mimba kulokea yai likirutubishwa na kutunza ujauzito. Kusipokuwa na kurutubishwa kwa yai ule utando ulioandaliwa hutoka kama damu ya hedhi.

Dawa za uzazi wa mpango zinakuwa na hormone za estrogen na progesterone.hivyo mwanamke anapotumia dawa za uzazi wa mpango zenye hormone hizi kiwango cha hormone hizi kwenye damu kinaongezeka na kufanya mwili kuhisi kuna kiwango cha kutosha cha hormone hizi hivyo kufanya tezi ya pituitari kuacha kuzalisha hormone chochezi ya mayai na hormone ya lutea.

Na kama tunavyojua yai haliwezi kupevuka kusipokuwa na hormone ya lutea na hormone chochezi ya mayai.

Mwanamke anapoacha kutumia dawa hizi inaweza kuchukua muda kwake kuanza kupevusha mayai na kupata siku zake kama kawaida.

Saa nyingi hali inaweza kuwa mtu anapata damu kidogo sana ya hedhi au mzunguko usioeleweka.

VIPIMO.
tatizo hili linaweza kugundulika kwa kupima kiwango cha hormone chochezi ya mayai (FSH) na hormone ya lutea kwenye damu.

MATIBABU
kitu cha kwanza ni kumshauri mtu alipata hali hii kusubiria kwa muda wa miezi 6,wanawake walio wengi ndani ya kipindi hiki cha miezi situ wanakuwa wamerudia katika hali yao ya kawaida.

Endapo imezidi miezi 6 au mwanamke ana uhitaji mkubwa wa mtoto basi kuna matibabu anapatiwa. Afike kupata ushauri wa daktari.