UGONJWA WA KISONONO - GONORRHEA

Ugonjwa wa Kisonono (Gonorrhoea) ni ugonjwa unaoshambulia watu wengi, wanaume kwa wanawake. Ni ugonjwa unaotibika ingawa kwa miaka ya karibuni, wadudu wa ugonjwa huu wameonyesha kuanza kutosikia tiba zinazotolewa. Kisonono kisipotibiwa kikamilifu, huweza kuleta madhara ya kudumu kwenye mwili wa mgonjwa na kumfanya aweze kuambukizwa au kuambukiza UKIMWI kwa urahisi. Katika ukurasa huu tutaona chanzo cha ugonjwa huu, dalili zake na mwisho kinga na tiba inayoweza kutolewa kwa ugonjwa huu. Chanzo Cha Kisonono (Gonorrhoea). Kisonono ni ugonjwa unaoambukiza kwa ngono – sexually transmitted infection (STI) – na unasababishwa na bakteria aitwaye Neisseria gonorrhoeae au gonococcus. Bakteria huyu hupenda kuzaliana kwenye maeneo ya joto, yenye unyevunyevu yakiwemo maeneo ya shingo ya uzazi (cervix), nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na mrija wa kutolea mkojo nje (urethra). Bakteria hawa pia huweza kuzaliana kwenye mdomo, mkundu na mara chache kwenye koo n...