NADHARIA ZA VIKOA VYA MAANA

Utangulizi Katika makala hii imegawanyika katika sehemu tatu, utangulizi, kiini na hitimisho. Utangulizi unajumuisha ufafanuzi wa nadharia ya vikoa vya maana, fasili mbalimbali ya vikoa vya maana pamoja na maelezo mafupi kuhusu vikoa vya maana pamoja na sifa za vikoa vya maana, katika kiini maelezo kuhusu umuhimu wa vikoa vya maana na mwisho ni hitimisho Nadharia ya vikoa vya maana imeasisiwa na Mjerumani Jost Strier (1930) akiegemea katika msingi wa kusema kuwa kuna maneno yanayofanana yanaweza kuwekwa pamoja. Mawazo haya ya Strier, Lyons (1970) anadai kuwa hayakuwa mawazo ya Strier bali yalikuwa ni ya Mjerumani mwenzake Von Hambolt. Wataalamu wengine waliokubaliana na mawazo ya Strier ni pamoja na Idsen, Jolls pamoja na Gao na Xu (2013). Hivyo basi, fasili ya vikoa vya maana imetolewa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo: 1.1 Fasili ya Vikoa vya Maana Resani (2014) anasema vikoa vya maana ni seti au kifungu cha maneno kilicho katika mpangilio fulani, au ni seti ya man...