NI Ijumaa nyingine nzuri tunapokutana katika uwanja wetu huu, kujadiliana kuhusu mambo yanayohusu uhusiano wa kimapenzi. Leo nataka tujadiliane kitu tofauti kwa lengo la kuwekana sawa. Napenda kuzungumza zaidi na wanawake. Kama wewe ni mwanamke, umewahi kujiuliza mumeo anahitaji nini zaidi kutoka kwako? Yawezekana likawa ni swali ambalo halina maana, lakini majibu yake ni mapana zaidi. Wengi huwa wanafikiri hitaji kubwa la mwanaume kwa mwanamke, ni kufanya mapenzi, lakini je, hilo ndilo jibu sahihi? Ipo wazi kwamba tendo la ndoa ndilo linaloikamilisha ndoa, iwe imefungwa Kikristo, Kiislam, kimila au kiserikali. Hakuna ndoa ambayo inaweza kukamilika bila wanandoa kukutana kimwili, lakini je, hilo ndilo hitaji pekee linaloweza kumfanya mumeo akaridhika na wewe? Wanawake wengi, hasa wasichana wanaoanza kuingia kwenye mapenzi, huhisi wao ni warembo, wana mvuto machoni mwa wanaume au wana maumbo mazuri, basi hiyo ndiyo tiketi ya wao kuolewa na kudumu kwenye ndoa zao. Hata hivyo,...