Posts

Namna ya kukabiliana na kikohozi kwa siku moja tu

Image
Vitunguu vinapendekezwa kwa hali ya upumuaji,ikiwa ni pamoja na kikohozi na homa. Endapo vikitumika vikiwa vibichi, ina aminika kuwa nzuri zaidi. Vina flavanoids na compaund za sulfur, ambavyo vinafanya Kitunguu kuwa na manufaa kwa moyo, viwango vya cholesterol, kisukari,arthris, na kwa ujumla kama antioxidant. Viungo. 1. Paundi moja ya vitunguu 2. Lita 3 za maji Njia za kufuata: Ondoa ngozi yote ya juu ya vitunguu,na kila kimoja kata vipande vinne,kisha weka vitunguu vyako kwenye sufuria yenye maji, na anza kuvichemsha. Chemsha maji kwa mda wa nusu saa, na kisha viache vipoe. Kunywa kikombe kimoja na nusu mara mbili kwa siku, ukipenda unaweza ukachanganya na asali na limao.

SAIKLOPEDIA NA KAMUSI

TOFAUTI BAINA YA SAIKLOPEDIA NA KAMUSI Kamusi na Saiklopidia ni dhana mbili zenye mkanganyiko mkubwa hasa katika suala zima la maana na matumizi. Aidha wataalam mbalimbali wametoa fasili ya dhana hizi ili kuweka bayana tofauti zilizopo baina ya Saiklopidia na Kamusi. Kwa mujibu wa  The Concise Oxford Dictionary of Current English , Saiklopidia ni kitabu kilichopangwa kialfabeti ambacho aghalabu hutoa taarifa juu ya masomo mbalimbali, au vipengele mbalimbali vya somo au mada moja. (Tafsiri yangu) Pia Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili (2000) inafafanua kwamba, ensaiklopidia ni kitabu au seti ya vitabu vinavyotoa taarifa kuhusu mambo mengi. Vilevile Mdee (2010) anasema saiklopidia ni kitabu chenye mkusanyiko wa makala zinazohusu nyanja anuwai za elimu ambazo hupangwa kialfabeti na kuandikwa maelezo ya kina kwa muhtasari. Mdee (Kashatajwa) akimnukuu Zgusta (1971) kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani, ...

SINTAKSIA NININI?

SINTAKISIA HAIWEZI KUTENGANISHWA NA VITENGO VINGINE VYA LUGHA. Katika kujadili mada hii, kwanza tutatoa fasili ya sintaksia kwa mujibu wa wataalam mbalimbali, fasili ya lugha, tutafafanua uhusiano uliopo kati ya sintaksia na vitengo vingine vya lugha na mwisho tutatoa hitimisho juu ya mjadala wetu. Kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999) Sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojihusishana uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake. Wanaendelea kusema, utanzu huu huchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika. Pia Habwe na Karanja (2004) wanasema Sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa sentensi na elementi nyingine zinazounda sentensi kama vile kategoria za maneno, vikundi na vishazi. Kutokana na fasili hizi inaonekana kuwa Massamaba na wenzake wamefafanua zaidi kwa kuonesha kuwa licha ya kuzingatia kanuni na sheri...

SHAABAN ROBERT NA MAANDIKO

MAANDIKO YA SHAABAN ROBERT Kwa mujibu wa waandishi na watafiti mbalimbali, mfano Sengo (1975), Kezilahabi (1976) na Gibbe (1980) wanasema kuwa jumla ya kazi alizowahi kuzitunga Marehemu Sheikh Shaaban Robert na zilizochapishwa hadi sasa ni ishirini na mbili, ambapo kumi na nne ni za ushairi na nane ni za nathari. Hata hivyo baadhi ya maandiko ya watafiti wa hivi karibuni mfano Mulokozi (2002) na Chuachua (2008) yanaonesha kuwa jumla ya maandiko ya Sheikh Shaaban Robert yaliyo kwisha kuchapwa hadi hivi sasa ni ishirini na nne. Ponera (2010) anaungana na Mulokozi (2002) na Chuachua (2008) kwa kuorodhesha vitabu ishirini na nne vya Sheikh Shaaban Robert vikiwa kumi na nne ni vya ushairi na kumi ni vya nathari. Ponera (2010) anavitaja vitabu hivyo vya ushairi kuwa ni:  1) MWAFRIKA AIMBA (1969), Nelson. Nairobi 2) ALMASI ZA AFRIKA (1971), Nelson, Nairobi  3) KOJA LA LUGHA (1969), Oxford, Nairobi 4) INSHA NA MASHAIRI (1967), Nelson, Nairobi 5) AS...

KADO AREJEA MTIBWA

Image
Kipa Shabani Kado amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Mtibwa Sugar. Kado amerejea kuichezea Mtibwa Sugar baada ya kuihama na kwenda Mwadui FC ya Shinyanga. Bosi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser ameithibitishia MASHELE BLOGkurejea kwa Kado. "Kweli Kado amerejea na amesaini mkataba wa miaka miwili," alisema

NAFASI YA KAZI KUTOKA WORLD VISION TANZANIA

Image
World Vision Tanzania MANAGER, MWANZO PROJECT Reference: 7646-17N24105 Location: Africa – Tanzania Town/City: Arusha Application Deadline Date: 01-Aug-17 Category: Programme Effectiveness Type: Fixed term, Full-time International Role: No – Only National applicants will be considered. Duration1-2 Years JOB DESCRIPTION Purpose of the position: To provide overall leadership and supervision in implementation of Mwanzo Integrated Development Project to ensure optimum impact, cost effective and maintain high level of excellence, accountability, reporting, monitoring and evaluation as per WVT approved policies, systems, procedures and donor requirements. Communicate World Visions Christian ethos and demonstrate a quality of spiritual life that is an example to others. Major Responsibilities. Provide overall leadership and management in the implementation of Mwanzo Project. Ensure program implementation is executed as per approved program documents (approved budget, work plans an...

NAFASI YA KAZI KUTOKA EXIM BANK (TANZANIA) LTD

Image
EXIM Bank(Tanzania) Ltd , an indigenous bank in Tanzania, ranking •5th in the country in terms of total assets, is engaged in providing commercial banking. services to the Retail, Mid & Large Corporate by offering a wide range of innovative products of international standards, in all verticals, including Corporate & retail lending, deposit, payment solutions, foreign exchange operations, cash handling services and other ancillary services etc. The bank is also present in Uganda, Union of Comoros & Republic of Djibouti. JOB Title:  Senior Relationship Manaqer – Chinese Desk RESPONSIBLE FOR:  Chinese Business Development/ Relationship portfolio management DEPARTMENT:  Investment Banking REGION:  Dar es Salaam, Tanzania with Travelling to Subsidiaries in Uganda, Djibouti and Comoros HOURS OF WORK: 8am – 5pm Monday to Friday. Additional hours as required by workload PURPOSE OF JOB The purpose of this role is to build, partner and sustain r...