Mapya Yaibuka Tena Kwenye Hukumu Ya Babu Seya Na Papii Kocha!!
Mapya Yaibuka Tena Kwenye Hukumu Ya Babu Seya Na Papii Kocha!! April 27, 2017 Hussein S. Omary Tumaini jipya! Mtoto wa kiume wa mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Mbangu Nguza ameibuka na kusema kuwa, mwaka 2017 ndiyo wa mwisho kwa baba yake na mdogo wake, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kuendelea kutumikia kifungo chao cha maisha jela. Akizungumza katika mahojiano maalum na Amani mwanzoni mwa wiki hii, Mbangu alisema kuwa, turufu ya mwisho ya hukumu ya ndugu hao ipo kwenye mikono ya Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) yenye makazi yake jijini Arusha ambayo kimsingi vikao vitatu vya awali vimeshakaa na kubaini kuwa, hukumu ya Babu Seya na Papii ilikuwa na kasoro. “Unajua watu hawafahamu, kule ambako hukumu ya mzee na bwana mdogo (Papii), ilipelekwa kuna hatua. Kwanza kabisa, wale majaji wanatoka nchi mbalimbali, kwa hiyo siyo kwamba wanakwenda tu Arusha na kupitia hukumu, hapana. “Kilichofanyika ni kwamba, kuna watu ...