MWANAFUZI AFARIKI ZIWANI

 

Mwanachuo wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha St. Augustine (SAUT), Mwanza, Boaz Sanga amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiogelea kwenye Ziwa Viktoria, tukio lililotokea jana, Mei 1, 2024.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mwanza, SF Kamila Laban, amesema kijana huyo alifikwa na mauti katika eneo la Sweya alikokuwa anaogelea na wenzake baada ya kuingia kwenye eneo lenye kina kirefu.

SACF Kamila amesema baada ya Zimamoto kufika eneo la tukio zoezi la kumtafuta liliendelea hadi usiku bila mafanikio na leo Mei 02, 2024 wamefanikiwa kuupata mwili wake pembezoni mwa mawe ziwani hapo

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?