Posts

Showing posts from May, 2024

Nimeteseka sana na mpenzi ila nimepata tulizo la moyo

Image
  Hapa duniani ni matarajio ya kila kijana awe wa kike au wa kiume atakapofikisha umri wa utu uzima ataweza kumpata mchumba mwema na kufunga naye ndoa. Nilidhamiria kupata mume atakayenipenda na kunithamini kila wakati na chochote kile kisije kikatutenganisha maishani mwetu, japo hayo yote hayakuweza kutimia kwa urahisi.  Kwa sasa nasema kama nisingeweza kukutana na wataalam, African Doctors wanaotatua mengi katika mahusiano na ndoa, basi nisingeweza kufikia ndoto zangu. Kabla sijasimulia safari yangu ya kumpata mchumba wangu kwa usaidizi wa African Doctors, ningependa utakapomaliza kusoma utembelee tovuti hii; www.african-doctors.com ili kufahamu mengi.  Nilipofikisha miaka18 nilianza kupata hamu ya kuwa kwenye uhusiano, nilimpata kijana mmoja kwa jina la James ambaye tulisoma naye katika moja wapo wa vyuo vikuu nchini Kenya. Urafiki wetu ulikua kwa haraka sana na kufikia kuwa wapenzi wenye kupendana sana.  Hata hivyo, sikuweza kugundua kuwa James hakuwa mwaminifu h...

JE: Kumwaga mbegu za kiume mara kwa mara husaidia kuzuia saratani ya tezi dume?

Image
Linapokuja suala la afya ya wanaume, saratani ya kibofu cha mkojo inachukua nafasi kubwa. Ni aina ya pili ya saratani inayogunduliwa kwa wingi kwa wanaume duniani kote, ikifuatiwa na saratani ya mapafu. Kwa sababu tezi dume ni kiungo cha uzazi ambacho kazi yake kuu ni kusaidia kuzalisha mbegu za kiume – yaani majimaji ambayo hubeba manii wakati wa mshindo. Watafiti kwa muda mrefu wamekuwa wakijiuliza kuhusu athari za mambo ya ngono kwenye saratani ya tezi dume. Je, kumwaga mbegu za kiume hukulinda dhidi ya hatari ya  Tafiti za Kisayansi CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Kuna ushahidi wa kuunga mkono swali hili. Utafiti uliofanywa katika kipindi cha miaka 33 iliyopita ulionesha kuwa tafiti saba kati ya 11 – ziliona kuna manufaa ya kumwaga mbegu dhidi ya saratani ya tezi dume. Vile vile, kumwaga manii kunaweza kuogeza kinga ya mwili ya kibofu na kupunguza hatari ya maambukizi – ambayo ndiyo chanzo cha kukuwa kwa saratani. Kumwaga mbegu za kiume pia kunaweza kupunguza shughuli za mfumo w...

KIMBUGA HIDAYA KUSABABISHA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI

Image
 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” kilichopo katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya Tanzania umeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya pwani ya Nchi ambapo hadi kufika saa tatu usiku wa tarehe 02 Mei 2024 kilikuwa umbali wa takriban Kilomita 402 Mashariki mwa pwani ya Mtwara.   Taarifa ya TMA imesema nguvu ya kimbunga HIDAYA imeendelea  kuimarika na kuwa kubwa zaidi hadi kufikia usiku huo kasi ya upepo katika kimbunga iliongezeka na kufika kilometa 110 kwa saa ambapo inatarajiwa kuendelea kuimarika zaidi katika kipindi cha saa 24 kutoka muda huo.  “Mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa baharini bado inaonesha uwezekano mkubwa wa Kimbunga “HIDAYA” kuendelea kusogea karibu kabisa na pwani ya Tanzania na kuendelea kuwepo hadi tarehe 06 mwezi Mei 2024 ambapo kinatarajiwa kupungua nguvu baada ya tarehe 6 Mei 2024” ——— imeeleza taarifa ya TMA.   Uwepo wa kimbunga “HIDAYA” karibu na pwani ya Tanzania unataraj...

MWANAFUZI AFARIKI ZIWANI

Image
  Mwanachuo wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha St. Augustine (SAUT), Mwanza, Boaz Sanga amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiogelea kwenye Ziwa Viktoria, tukio lililotokea jana, Mei 1, 2024. Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mwanza, SF Kamila Laban, amesema kijana huyo alifikwa na mauti katika eneo la Sweya alikokuwa anaogelea na wenzake baada ya kuingia kwenye eneo lenye kina kirefu. SACF Kamila amesema baada ya Zimamoto kufika eneo la tukio zoezi la kumtafuta liliendelea hadi usiku bila mafanikio na leo Mei 02, 2024 wamefanikiwa kuupata mwili wake pembezoni mwa mawe ziwani hapo