Moto mkubwa wateketeza majengo Kariakoo

 

Moto huo umetokea asubuhi ya Oktoba Mosi, 2023 eneo la Kariakoo Dar es Salaam ambapo umeripotiwa kuwaka kwenye zaidi ya Majengo 5 yenye Maduka likiwemo la Jengo la Big Bon ambalo ndani yake kuna ofisi za Bank of Africa (BoA)

Imeelezwa Moto ulianzia eneo la Mnadani na kusambaa kwenye majengo mengine likiwemo jengo la Ghorofa 9 ambapo pia umeteketeza ghala la Pikipiki na baadhi ya Nyumba za Makazi ya Watu

Jeshi la Zima Moto linaendelea na zoezi la uzimaji pamoja na kufanya uokoaji, hadi sasa bado haijafahamika athari za Kibinadamu na hasara iliyotokana na Moto huo. Endelea kufuatilia kurasa zetu, taarifa zaidi zitakujia muda mfupi ujao.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?