MAHAFALI UDSM IDADI YA WAHITIMU WANAWAKE YAONGEZEKA JK ATOA NENO




 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne @jakayakikwete  amefurahishwa baada ya kuona idadi ya wahitimu wanawake chuoni hapo kufikia asilimia 54.7 na kuwashauri wanafunzi wanaume wafanye juhudi ili wasiachwe mbali sana na wenzao.

Akiongea kabla ya kuhitimisha duru la pili la mahafali ya 53 ya chuo hicho, Dkt. Kikwete amesema kwamba kafurahishwa na kuona wanawake siku hizi wakiupiga mwingi na kuwataka vijana wa kiume walichukulie jambo hilo kama changamoto kwa wao kufanya vizuri zaidi kwenye masomo.

 Katika mahafali hayo yalifofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jumla ya wahitimu 2796 walihudhurishwa ambapo 2700 walitunukiwa shahada za awali ikiwa ni wasichana 1488 na wavulana 1212.

Jumla ya Stashahada 78 zilitolewa kwa wanaume 45 na wasichana 33, wakati wanaume 10 na wasichana wanane walitunukiwa Astashahada

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?