Kocha kiboko wa Yanga apewa mkono wa kwaheri
Klabu ya Ihefu ‘Mbogo Maji’ inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC, imempa mkonoo wa kwaheri kocha wake, Zuber Katwila.
Katika taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo leo, Oktoba 14, 2023, Ihefu imeeleza kuwa uongozi wa timu hiyo umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba na kocha huyo.
“Hata hivyo uongozi wa timu unamshukuru Kocha Katwila kwa wakati wote aliokua nasi ndani ya timu kama Kocha Mkuu tangu alipojiunga nasi mwaka 2020,” imesomeka taarifa ya klabu hiyo.
Katwila akiwa Ihefu, amefanikiwa kuwafunga Yanga mara mbili mfululizo katika Uwanja wa Highland Estates, Mbarali ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni msimu uliopita alipovunja ‘unbeaten’ ya Yanga na msimu huu
Comments
Post a Comment