Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.11 ya mwaka 1995, na ilianza 

kufanya kazi tarehe 1 Julai 1996. Katika kutekeleza majukumu yake TRA inaongozwa na sheria 

na ina jukumu la kusimamia kwa uadilifu ukusanyaji wa kodi mbalimbali za Serikali. TRA 

inatekeleza mpango kazi wa sita (CP6:2022/23 - 2026/27) ikitekeleza Dira ya kuwa ‘‘Taasisi ya 

Mapato Inayoaminika kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi’’ na Dhamira ya ‘‘Kurahisisha na 

Kuimarisha Ulipaji Kodi wa Hiari kwa Maendeleo Endelevu’’

TRA inapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuanzia tarehe 27 Mei 2023 

mpaka 09 Juni, 2023 kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kwa hatua mbalimbali kuanzia tarehe 

24 September, 2023 na hatimaye kuwapatia barua ya ajira waombaji kazi watakaofaulu. 

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo: -

1. Usaili utafanyika kama ilivyooneshwa kwenye ratiba ikianisha siku, muda na sehemu. 

2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.

3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: - Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha 

Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au Hati ya kusafiria.

4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia Cheti cha Kuzaliwa, 

Kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana 

na sifa za Mwombaji. 

5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za 

matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA 

HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi. 

7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili. 

8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na 

kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA).

9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa 

hawakukidhi vigezo vya awali. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi 

zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika. 

10. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na 

vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi. 

11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na 

kunakili namba za usaili kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

12. Msailiwa haruhusiwi kuja na simu, saa au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye eneo la 

usaili. 

13. Ratiba ya Usaili inapatikana kupitia www.tra.go.tz

Kwa taarifa Zaidi, tembelea Ofisi za TRA zilizo karibu nawe au tumia mawasiliano yafuatayo:

Tovuti

: www.tra.go.tz

Namba za simu bila malipo : 0800 780078 au 0800750075

WhatsApp

: 0744 23 33 33

Barua pepe

: huduma@tra.go.tz au services@tra.go.tz

‘‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’’

Imetolewa na;

Idara ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala

Bofya Tangazo kupakua majina