FALSAFA YA UBUNTU NA FAIDA ZAKE KATIKA JAMII

 Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Falsafa hii inaonesha nafasi ya mtu katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kama jamii kuliko ubinafsi. (Kwa mujibu wa Wikipedia)

Sanamu ya tembo yenye mchoro wa Ubuntu, Florianópolis, Brazil

Neno Ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu na Kixhosa za Afrika Kusini. Neno la Kihaya "Obuntu" au kwa Kiswahili "utu" linabeba, kwa kiasi fulani, maana ya neno Ubuntu.

Falsafa ya Ubuntu imetokana na mila na utamaduni wa Kiafrika ambao umejengwa juu ya maslahi ya jamii zaidi ya maslahi ya mtu binafsi.

Msingi wa falsafa hii ni, "mtu si mtu bila watu," kwa Kizulu, "Umuntu ngumuntu ngabantu." Kwa Kihaya "Omuntu ti muntu ka ataliho bantu" kwa kichagga , "mndu Ni mndu ku bila Vandu" Baadhi ya watu wanaiona falsafa ya Ubuntu kuwa na maana nzito ya kiroho na ya kidini kwa kuwa imejengwa juu ya upendo wa watu wengine (kama unavyojipenda wewe) na hata mazingira.

Faida za falsafa ya Ubuntu katika jamii

1. Kuchochea uwajibikaji

2. Kuchochea maendeleo ya jamii

3. Utawala Bora

4. Umoja na mshikamano


Swali la mjadala : Jadili kwa kina Falsafa ya Ubuntu inavyoweza kuwa mkombozi wa nchi ya Tanzania na Africa kwa ujumla.

Swali la pili: Jadili Mimi sii Mimi bila wewe  inavyoweza kuleta amani duniani

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?