USAJILI MPYA : SAMATTA ASAJILIWA PAOK FC

 

 

Nyota wa soka kutoka Tanzania anayekipiga kimataifa, Mbwana Ally Samatta, amesajiliwa na timu ya PAOK FC ya nchini Ugiriki ambapo leo ametambulishwa rasmi.

Kupitia akaunti za mitandao ya kijamii za timu hiyo, Samatta amepostiwa leo, ikielezwa kuwa atakuwa akivaa jezi namba 33.

Kabla ya kwenda PAOK, Samatta alikuwa akiichezea Genk ya Ubelgiji kwa mkopo, akitokea Fenerbahce ya Uturuki.

Safari ya soka ya Samatta ilianzia katika timu ya Mbagala Market kabla ya kuhamia Simba na baadaye akatoboa kimataifa ambapo mpaka sasa anaendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?