USAJILI SIMBA : BALEKE KWENDA ULAYA?

 

Jean Baleke

UONGOZI unaomsimamia Jean Baleke umeweka wazi kuwa umepokea ofa kutoka kwa timu nyingi zikiwemo zinazocheza katika ligi mbalimbali barani Ulaya.

Jean Baleke ambaye anakipiga katika klabu ya Simba kwa mkopo akitokea TP Mazembe amekuwa akifanya vyema ndani ya Simba tangu atue amefunga mabao nane katika mechi nane alizocheza kwenye ligi jambo ambalo mashabiki wengi wamekubali uwezo wake.

Akizungumza na Championi Jumatano, Faustino Mkandila ambaye ni moja kati ya wasimamizi waliomleta Simba mchezaji huyo ameweka wazi kuwa juu ya timu kutoka Ulaya zikiwa zinamhitaji mchezaji huyo kupitia dirisha kubwa jambo ambalo lazima Simba wafanye kazi kubwa kumbakisha mshambuliaji huyo.

“Baleke yupo Simba kwa mkopo hivyo Simba wanatakiwa kufanya kazi kubwa sana kumbakisha Baleke kutokana na timu nyingi kumnyatia haswa kutoka Afrika na Ulaya.

“Tayari timu nyingi zimeleta ofa ya kumhitaji Baleke hadi timu kutoka ligi za Ulaya wameonekana kuvutiwa na uwezo ambao ameuonyesha hivyo kuna kazi kubwa lazima itumike kwa Simba kama watahitaji kuendelea kuwa na Baleke kutokana na uwezo mkubwa alionao,” alisema kiongozi huyo.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?