KIJANA ALIYELALA MZIMA NA KUAMKA KIPOFU ASIMULIA MAZITO
KIJANA anayejulikana kwa jina la Alphaxad Robert amesimulia mkasa wa maisha yake baada ya kupofuka macho alipokuwa na umri wa miaka 11.
Alpha anasema siku moja ya Ijumaa asubuhi aliamka lakini aligundua kuwa alikuwa hawezi kuona kitu chochote ambapo aliamua kuwataarifu wazazi wake na wakaanza jitihada za kumtibia sehemu tofauti tofauti ikiwa ni hospitali pamoja na kwa waganga.
Ilimchukua miaka 4 kutibiwa lakini hakufanikiwa kupona na amekuwa kipofu mpaka leo na mambo yake yanaenda vizuri, kwani tatizo lake la macho halikumfanya akate tamaa.
Video Credit : GP
Comments
Post a Comment