Habari kubwa kimataifa Leo jioni Juni 26/2023

 


Jioni katika Dunia Yetu:

👉Licha ya ikulu ya Urusi, Kremlin, kusema hakungekuwa na mashtaka dhidi ya kiongozi wa kundi la kijeshi la Wagner (pichani) na wapiganaji wake, duru kutoka nchini humo zinasema uchunguzi wa uhalifu dhidi ya kiongozi wake Yevgeny Prigozhin bado unaendelea. Prigozhin alielezwa kwenda uhamishoni nchini Belarus kufuatia upatanishi wa rais wa nchi hiyo Alexander Lukashenko. Ripoti zinasema Prigozhin ameonekana mjini Minsk, ambao ndiyo mji mkuu wa Belarus.


👉Suala la uasi wa kundi la mamluki la Urusi la Wagner linatarajiwa kutawala ajenda kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya unaofanyika leo nchini Luxemburg. Kando na kadhia ya vita vya Ukraine, mkutano huo pia utajadili jinsi ya kushughulikia mizozo inayotokea ndani ya Umoja huo.


👉Wapiganaji wa kundi la jihadi la Al-Shaab wameripotiwa kuwauwa raia watano, baadhi kwa kuwakata vichwa mashariki mwa Kenya kwa mujibu wa mashuhuda na duru za Polisi. Je, kundi hili linapata wapi tena nguvu za kufanya mashambulizi licha ya juhudi kubwa za kikanda na kimataifa kulitokomeza? Wapi wanakosea?


👉Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI, imefungua milango kwa wagombea wa nafasi za ubunge kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo, kupitia jumla ya ofisi 171 kote nchini, huku pia ikitangaza kuahirisha hadi tarehe ambayo haijataja, uandikishaji wa wapigakura katika eneo la Kwamouth mkoani Mai-Ndombe.


👉Kiongozi wa chama cha kihafidhina nchini Ugiriki Kyriakos Mitsotakis amekabidhiwa madaraka ya kuhudumu muhula wake wa pili hii leo Jumatatu baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika jana Jumapili, ambao ulikuwa wa pili katika kipindi cha wiki tano.

Via DW

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?