AMUUA BABA YAKE KISHA KUMPIKA KAMA MBOGA

Mwanaume mmoja kutoka kijiji cha Giankaja, kaunti ya Tharaka Nithi alitiwa mbaroni baada ya kudaiwa kumuua baba yake na kupika sehemu za mwili wake. Mwanamume huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi kaunti ya Tharaka Nithi nchini Kenya. Polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha wakisema mwathiriwa ambaye ni mzee mwenye umri wa miaka 70, aliripotiwa kutoweka kwa siku tatu. Msako ulifanyika katika kijiji kizima na wakazi wa eneo hilo katika juhudi za kumtafuta mzee huyo. Baada ya saa kadhaa za msako, upekuzi wao uliwaelekeza kwenye mtaro wenye kina kirefu ambapo waliupata mwili wa marehemu ambao tayari ulikuwa umeshaanza kuoza. Marehemu alikuwa amekatwa kichwa na sehemu za mwili wake kukatwa na miguu yake ikiwa kando ya mwili wake. Walikimbia haraka kwa chifu wa eneo hilo ili kumjulisha kuwa wamempata mtu aliyepotea. Hata hivyo, waliporejea kwenye mtaro, mwili huo haukuonekana. Wakiwa wamechanganyikiwa na jinsi mambo yalivyobadilika, wenyeji hao kat...