Skip to main content

Video ya DJ Brownskin Akimrekodi Mkewe Akinywa Sumu


Julai 29, 2022, mwanadada Sharon Mwangi alifariki dunia na wiki moja baadaye akazikwa; Watu wasijue kuwa kuna tukio lilitokea alilolirekodi mume wake aitwaye Hamisi Ramadhan au DJ Brownskin.
DJ kwenye msiba wa mke wake

Hivi karibuni video imevuja ikimuonyesha DJ akimtazama mkewe akinywa sumu mbele ya watoto wao…..Sharon akajilaza kwenye sofa huku Dj akiendelea kurekodi. Mtoto wao anaonekana kwenye video ingawa hajui kinachoendelea. Dj Brownskin baadaye akampigia simu msaidizi wao wa nyumbani ampe mke maziwa.

Siku ya msiba DJ aliandika “Kifo chako kiliacha pengo maishani mwangu ambalo ninalijaza na upendo tulioshiriki.”

Wadau wamekuwa na mitazamo mbalimbali huku wengi wao wakimlaumu mwanaume. Wengine wanadai kuwa ukitazama video hiyo ni wazi walikuwa na migogoro mingi, hasa mama huyo alivyokuwa akikataa kunywa Maziwa. Kwa hiyo ni vyema kumpa DJ nafasi aeleze kisa kizima kabla ya kumhukumu.

Kulingana na sheria za Kenya, ukipatikana na hatia ya kusaidia mtu kujitoa uhai . Kifungo ni cha maisha jela.

Credit: mcshondelive

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?