SIMBA KUKUTANA NA MABINGWA HAWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 

Kikosi cha timu ya Simba.

KESHOKUTWA Jumatano Simba iatafahamu ni nani ambaye watakutana naye kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati ambao droo ya hatua hiyo itakuwa inapangwa kule Misri lakini ni lazima waangukie kwa moja ya vigogo wa Afrika.

Simba wametinga hatua hiyo mara baada ya kumaliza nafasi ya pili katika kundi C ambalo lilikuwa na timu za Raja Casablanca, Vipers, Horoya AC na wao.

Championi Jumatatu limefahamu timu ambazo zina nafasi kubwa ya kukutana na Simba katika hatua hiyo kutokana na jinsi ambavyo droo ya michuano hiyo inachezeshwa.

Kwa mujibu wa upangaji wa timu zinavyokutana, huchukuwa zile timu nne zilizoongoza katika kila kundi kisha kuchezeshwa droo na timu nne zilizoshika nafasi ya pili kwa ajili ya kupata timu nane zitakazokutana.

Hivyo Simba ambaye ameshika nafasi ya pili atakuwa katika poti moja na timu nyingine tatu ambazo zimemeliza katika nafasi ya pili katika makundi yao kama Al Ahly, JS Kabyile na CR Belouzidad ambapo watacheshwa droo na timu zilizoongoza makundi ambazo ni Wydad Casablanca, Mamelodi Sundowns, Raja na Espérance.

Stori na Marco Mzumbe

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?