ICC YATOA HATI YA LUKAMATWA PUTIN

 

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) Machi 17, 2023 imetoa hati ya kumkamata Rais wa Russia Vladimir Putin, ikimshtumu kuwa muhusika mkuu wa uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Moscow ilikanusha mara kadhaa tuhuma kwamba wanajeshi wake walifanya ukatili katika uvamizi wa Russia dhidi ya jirani yake ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.

ICC imetoa hati ya kumkamata Putin kwa tuhuma za kuwahamisha kinyume cha sheria watoto na raia wengine wa Ukraine hadi Russia.

Mapema wiki hii, shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba ICC ilikuwa inatarajiwa kutoa hati kadhaa, kwa mara ya kwanza katika uchunguzi wake juu ya mzozo wa Ukraine.

Mahakama hiyo imetoa pia hati ya kumkamata Maria Alekseyevna Lvova-Belova, Kamisheni wa haki za watoto wa Russia, kwa shutuma hizo hizo zilizotolewa dhidi ya Putin.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?