falsafa ya kiafrika katika riwaya za kiethnografia za kiswahili
![]() |
Lameck mpalanzi PhD UDSM photo credit www.udsm.co. ac |
Lameck Mpalanzi
Tasinifu ya Ph.D Kiswahili
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Institute of Kiswahili, 2019
Utafiti huu unachunguza ujitokezaji wa vipengele vya falsafa ya Kiafrika katika riwaya teule za
Ethografia ninini?
Ethnogafia ni tawi mojawapo la anthropolojia na uchunguzi wa kimfumo wa tamaduni za mtu binafsi. Ethnografia inachunguza matukio ya kitamaduni kutoka kwa mtazamo wa SoMo la utafiti
kiethnografia za Kiswahili. Vipengele vilivyochunguzwa ni dini ya jadi, uganga na uchawi, uzazi, uhai na
kifo na uduara wa maisha. Katika kuchunguza vipengele hivyo, riwaya zilizoteuliwa na kuchambuliwa ni
Kurwa na Doto, Mirathi ya Hatari na Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka; Ntulanalwo na Bulihwali.
Vilevile, utafiti ulilenga kubainisha namna vipengele teule vilivyomo katika riwaya vinavyoakisiwa katika
jamii teule za Unguja, Njombe na Ukerewe. Aidha, utafiti ulilenga kuchunguza mwingiliano wa riwaya ya
kiethnografia ya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika. Kadhalika, utafiti unafafanua mehango wa falsafa ya
Kiafrika katika maendeleo ya fani na maudhui ya riwaya teule. Katika kukamilisha malengo haya, data
ilikusanywa maktabani na uwandani kwa kutumia mbinu ya udurusu wa maandiko maktabani,
mahojiano, hojaji, ushuhudiaji na ushiriki. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili kuanzia nyakati za
ukusanyaji data hadi uchambuzi. Nadharia ya kwanza inaitwa Ontolojia ya Kibantu, na ya pili Sosholojia
ya Fasihi. Ontolojia ya Kibantu ilituongoza kuchambua masuala yanayohusu falsafa yaKiafrika na
Sosholojia ya Fasihi ilitusaidia kuhakiki masuala yanayohusu uhusiano wa fasihi na jamii. Matokeo ya
utafiti huu yanaonesha kuwa fasihi hubeba falsafa ya jamii kwa kuwa vipengele teule vya falsafa ya
Kiafrika vinadhihirika bayana katika riwaya teule. Utafiti umethibitisha kuwa tambiko linachukua sehemu
kubwa ya dini ya jadi, ambayo ndiyo mzizi wa imani ya Waafrika. Jamii hizi zina matambiko mengi,
mathalani, jamii ya Wamakunduchi ina tambiko is Mwaka-kogwa, tambiko la kumaliza msiba,tambiko la
uzazi, tambiko la unyago na tambiko la mazishi. Jamii ya Wabena ina tambiko la kafara (Kipongo),
Nyumbanitu na Amalimilo. Kwa upande mwingine, Wakerewe wana tambiko la kuzaliwa, uzazi na
kutanabahi katika pembe, tambiko la kumtoa mtoto nje,tambiko la harusi, tambiko la kuvundika ndizi,
tambiko la ugonjwa na tambiko la mazishi. Pia, Wakerewe, wana tambiko la machifu huko Kitare,
tambiko katika makumbusho ya Handebezyo na katika "Jiwe Linalocheza." Utafiti umebaini kuwapo kwa
imani mseto katika jamii teule inayotokana na mwingiliano wa dini ya jadi na dini za kigeni. Kuwapo kwa
imani mseto ni jitihada za jamii teule kutafuta utambulisho na ukubalifu wa kila kundi. Utafiti umebaini
kuwa upo mpaka bayana kati ya fani ya uganga na uchawi kwa kuzingatia kigezo cha utendaji, dhima,
kiwango cha nguvu-hai, miiko na ufantasia wa fani hizo. Uchunguzi katika riwaya na jamii teule umebaini
kuwapo kwa makundi kumi (10) ya waganga na makundi mawili (2) ya wachawi. Utafiti unaonesha kuwa
baadhi ya waganga na wachawi wanaishi maisha duni kwa kuwa hutumia gharama kubwa kununua
viambato vya uganga na uchawi. Licha ya kufumbata falsafa mbalimbali za maisha, suala la uzazi katika
jamii ya Ukerewe ni mfano dhahiri wa kuwapo kwa familia pana ya Kiafrika inayojumuisha watu-hai,
waft' na watakaozaliwa. Sanjari na hilo, utafiti huu unaafiki kuwa kifo kwa Mwafrika si mwisho wa
maisha kwani mfu huendelea kuwapo kama inavyoelezwa katika Ontolojia ya Kibantu. Hata hivyo, utafiti
unaonesha kuwa maisha ya maana na halisi ni ya hapa duniani. Aidha, utafiti huu ulibaini kuwapo kwa
uhusiano wa kiduara kati ya mtu, jamii na mfumo uliopo. Kiontolojia, utafiti umethibitisha kuwapo
uhusiano wa kiduara kati ya Mungu, mizimu, wahenga, binadamu, wanyama na mimea, na vitu na
mahali. Katika kudhihirisha fasihi inavyobeba falsafa ya jamii, utafiti huu umetambua kuwa fasihi na
falsafa ya Kiafrika hutenda majukumu yanayofungamana. Mwisho, utafiti huu unabainisha kuwa falsafa
ya Kiafrika ni malighafi na nyenzo muhimu katika uandishi wa fani na maudhui ya riwaya ya Kiswahili.
Comments
Post a Comment