Jina langu ni Nasra kutokea Tanga nchini Tanzania, miaka kadhaa nyuma iliyopita nilijikuta kwenye sehemu ya mauzauza, nilikuwa naota ndoto mbaya, nilikuwa katika mazingira ya shule, kwa kuwa mazingira yale yalijaa mauzauza sikuweza kushangaa sana. Ilikuwa haipiti wiki mimi sijaugua, nilikuwa naota ndoto kama nakabwa, kipindi hicho bado nipo Shule, ilikuwa ni hali ya kuhatarisha katika maisha yangu, kiukweli katika dua na jamaa zangu lakini haikusaidia lolote. Tulikuwa tunaamka pamoja na rafiki yangu muda wa saa 11 alfajiri, tunaomba dua hadi saa 12 asubuhi, kisha tunakwenda kuungana na wenzetu. Usiku saa nne kamili tunaanza dua walau nusu saa kisha tunakwenda kulala. Siku moja nakumbuka ilikuwa Ijumaa kuamkia Jumamosi, kama kawaida yetu baada ya prepo tulikwenda kufanya dua kwenye kajumba ambako kalikuwa kama mita 50 toka mabweni yalipo. Wakati tunaendelea kupiga dua ya nguvu, tukiwa tumeshikana mikono, ghafla ulijitokeza moto unaowaka katikati yetu, kwa kuwa ma...