Editors Choice

3/recent/post-list

Chupa za maji za plastiki zinaweza kusababisha saratani?

 


Maji

Chanzo cha picha, Getty Images

Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu chupa na vifungashio vya chakula vya plastiki kusababisha saratani. Yapo madai yanayozunguka kuhusu kemikali hatari katika vifungashio vya plastiki vinavyotumika kwa baadhi ya vyakula na vinywaji.

Inadaiwa Wakati chupa za maji ya kunywa zikiwekwa kwenye jua, miale ya jua inasababisha vitu vilivyo kwenye plastiki kuyeyuka ndani ya maji, na kisha kemikali zinazotengenezwa kutoka kwa plastiki zitafyonzwa na maji ya kunywa ya mtu. Hii inasababisha saratani.

Mjadala huu umechochewa zaidi na barua pepe iliyoandikwa na mtafiti wa chuo kikuu ambayo ilisambaa mitandaoni. Barua pepe hii imekuwa ikitajwa sana kwenye tafiti kadhaa.

water

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata hivyo, wanasayansi wa afya wamepinga hoja hiyo ya mtafiti na kumekuwa na wasiwasi kuhusu ukweli wa kisayansi kuhusu kemikali inayoitwa bisphenol A, au BPA.

Wanasayansi wanasema mifuko, chupa ama vifungashio vya plastiki vinakuja na kemikali hii na inaweza kuwa na madhara kwa afya. Uchunguzi unaonyesha kuwa kemikali ya BPA inaweza kuathiri mfumo wa homoni za kike.

Water

Chanzo cha picha, Getty Images 

Lakini swali ni je, kuna ushahidi wowote kwamba kemikali hizi ni hatari?

Kemikali hizi zinaweza kuathiri panya wadogo iwapo watapew akemikali hiyo kwa wingi.

Ingawa mfumo wa usagaji chakula wa binadamu hushughulika na kemikali hizi tofauti na viungo vingine.

Plastiki iliyotengenezwa na kemikali ya BPA imekuwa ikitumika kwa miaka mingi. Bado hakuna ushahidi dhabiti unaoonyesha jinsi BPA inavyoathiri miili yetu kila siku na jinsi inavyoathiri afya yetu kwa ujumla.

Utafiti mwingine unaonyesha kuwa BPA hupatikana kwenye mkojo wa watu wazima wengi katika nchi zilizoendelea.

Athari za kemikali hizi zinaweza kuzuiwa kwa kutotumia BPA kwenye mifuko ya plastiki au vyombo. Plastiki au mifuko mingi huwa na nambari iliyochapishwa inayoonyesha ni kiasi gani cha kemikali hiyo kilichomo.

Je, unaitambuaje BPA kwenye vifungashio?

Water

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Nambari hizi zinaweza kutambuliwa kwa ishara ya pembetatu (♲).
  • Kama kuna BPA huwekwa herufi na namba A3 au 7 na ikiwa hakuna BPA katika alama hii (♲) hufuatia na namba 1, 2, 4 au 5.
  • BPA hutokea wakati plastiki ikiguswa ama kikipata joto.
  • Hata hivyo, tafiti zimethibitisha kuwa majaribio yaliyofanywa kwenye vifungashio vya plastiki kama chupa za maji hazina BPA. 
Chanzo:  BBC

Post a Comment

0 Comments