ASILIMIA 10 YA KODI YA PANGO YAWA GUMZO:
Wakati suala la wapangishaji wa nyumba kutakiwa kulipa asilimia 10 ya kodi yao kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) likizidi kuwa gumzo nchini, Serikali imesema itaendelea kutekeleza matakwa ya sheria hiyo huku pia ikipokea maoni ya wadau.
Wakati huo huo Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imetoa ufafanuzi juu ya kodi ya pango kwa kueleza siyo kodi mpya bali imeongezwa wigo kutoka kwenye nyumba za biashara hadi nyumba za kawaida za kupangisha.
TRA imesema mabadiliko haya yametokea kwenye kifungu cha 82(2)(a) cha sheria ya kodi ya mapato sura 332 kilichokuwa kinawataka wapangaji ambao ni wafanyabiashara wawakate wenye nyumba asilimia 10 ya pato.
Na kwa mabadiliko hayo, sasa kipengele hicho kitamtaka kila mwenye nyumba anayepangisha aweze kuchangia Serikali 10 ya mapato yake ya ada za pango.
Nini maoni yako katika utekelezaji wa Takwa hili la Sheria?
Comments
Post a Comment