Shirika la Afya Duniani Latangaza Homa ya Nyani Kuwa Tishio la Afya Ulimwengun



                                  

SHIRIKA  la Afya Duniani WHO limeutangaza mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nyani ambao tayari umeathiri zaidi ya watu 17,000 katika nchi 74 duniani kuwa dharura ya afya ya ulimwengu.

 

Hiyo ni tahadhari ya juu kabisa inayoweza kutolewa na shirika la WHO kuhusu dharura yoyote ya kiafya ulimwenguni.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Geneva amesema  kwamba ameamua kuitangaza Homa ya Nyani kuwa dharura ya kiafya duniani baada ya timu ya wataalamu kushindwa kufikia makubaliano.

 

Amesema tathmini ya WHO inaonyesha kitisho cha Homa ya Nyani duniani bado ni cha wastani isipokuwa barani Ulaya ambako visa vya maambukizi vinaongezeka

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?