JINSI YAKUJUA TAREHE YAKO YAKUJIFUNGUA
Mwanamke anatakiwa kujua tarehe yake ya kujifungua ili aweze kujiandaa, hata hivyo ni muhimu sana wewe na mpenzi wako kufahamu ni lini unatarajia kupata mtoto ili kutoa muda wa kufanya maandalizi ya kifedha na namna ya kujifungua.
Umri wa ujauzito ni miezi au wiki ngapi?
Wastani wa kipindi cha ujauzito ni siku 280 ama wiki 40 kamili kwa binadamu.
Njia gani hutumika?
Ili kujua tarehe yako ya kujifungua, njia inayotumika kujua tarehe yako inaitwa Naegele's rule.
Njia hii hutumika mara nyingi kwa mwanamke mwenye mzunguko usio badilika badilika sana na unachukulia mwanamke anaona hedhi baada ya siku 28 na katikati ya mzunguko wake ni siku 14. Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35 siku yake ya katikati ni siku ya 21
Tarehe ya matazamio inagunduliwa kwa, kwanza kujua tarehe yako ya mwisho ya siku ya kwanza kuaona damu ya mwezi. Kisha;
- Ongeza 7 kwenye tarehe, toa 9 /ama 3 kwenye mwezi kwa mzunguko wa siku 28
- Ongeza 0 tu kwenye mzunguko wa siku 21
Ongeza 14 kwenye tarehe kwa mzunguko wa siku 35
Mfano kama mwanamke mara ya mwisho kuona siku zake ni tarehe 21/3/2008 hivyo tarehe ya matazamio ni
siku mwezi Mwaka
21 3 2008
+ 7 +9
28 12 2008
Kama siku yake ya mwisho kuona damu ni 21/5/2008
siku mwezi mwaka
21 5 2008
+ 7 -3
28 2 2008
Na ikiwa mwanamke ameona siku yake ya mwisho tarehe 25/6/2015 tarehe yake ya matazamio ni
siku mwezi mwaka
25 6 2015
+7 -3
2 3 2016
Kama hujaelewa mahesabu haya Wasiliana nasi whatsapp 0762167811 kupata maelezo zaidi. Endapo una shida yoyote kiafya unahitaji kuongea na daktari wasiliana nasi whatsapp 0657282717
Comments
Post a Comment