ROMBO: AUAWA AKIMENDEA ASALI YA WENYEWE, MUUAJI AJISALIMISHA POLISI

 

 


Mkazi wa kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Juvenal Claudi (20) ameuawa kwa kukatwa katwa na mapanga baada ya kufumaniwa akitaka kufanya mapenzi na na mke wa mtu.


Taarifa zinadai kuwa kijana huyo aliyeuawa alikuwa akichati na mke wa mtu ambapo baadaye mume wa mwanamke huyo, Riziki Shirima (22) alidaka simu ya mkewe na kukuta meseji za mapenzi.


Baada ya kukuta meseji hizo, mwanaume huyo aliweka mtego kwa kuendelea kumtumia meseji kijana huyo aliyeuawa, akijifanya yeye ndio mwanamke huku akimtaka kuja nyumbani jambo ambalo alifanya hivyo.


Baada ya kijana huyo kufika nyumbani alianza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na baadaye kufariki dunia.


Kamanda wa Polisi Mkoani wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema tukio lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 4 na kusema baada ya mwanaume huyo kufanya mauaji alijisalimisha mwenyewe polisi.


"Ni kweli hili tukio limetokea katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo ambapo mwanaume alimfumania mkewe nyumbani kwake akiwa na huyu kijana aliyeuawa wakitaka kufanya mapenzi," amesema Kamanda Maigwa


Kamanda Maigwa amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia muuaji baada ya kujisalimisha mwenyewe polisi.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?