Posts

Showing posts from December, 2021

Job Opportunities at ICAP, Field Officer ( Multiple Positions)

Image
Field Officers ( Multiple Positions)  Job no: 495846 Work type: Regular Full-Time Location: Tanzania – Mwanza Categories: Program Management/Implementation/Support, Technical/Clinical/Quality Improvement/Training ICAP at Columbia University, a global health leader situated within the Columbia University Mailman School of Public Health in New York City, seeks highly qualified candidates to serve as Field Officer, based in Mwanza Tanzania. Reporting to the Community Coordinator, the Field Officer is responsible to manage the day-to-day field implementation community-based HIV services in the intervention district, focusing on HIV testing and prevention activities such as DREAMS, PrEP, condom programming, peer-based outreach, among others. Supervising field assistants, the team will work alongside healthcare providers and peer volunteers. The position is contingent upon availability of grant funding. Columbia University is an equal opportunity and affirmative action emplo...

Polisi: Mhitimu wa SUA Aliyeuawa, Alivutwa Shingo

Image
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kufuatia kifo cha mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Magreth Mashue, na kusema kwamba uchunguzi wa awali wa daktari umebaini kwamba shingo ya marehemu ilivutwa.   Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro Ralph Meela, na kusema kwamba waliyemkamata ni mwanachuo mwenzake aliyekuwa akiishi naye.   Imeelezwa kwamba Magreth alipotea Desemba 14 hadi Desemba 18 mwili wake ulipopatikana katika mashamba ya chuo hicho.

VILIO, SIMANZI VYA TAWALA, MWILI WA MWANAFUNZI SUA ALIYEUAWA UKIAGWA MORO

Image
  Vilio na Simanzi vimetawala wakati wa ibada ya kumuaga Mwanafunzi ambaye amehitimu katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro, Magreth Mashuwe aliyeuawa na watu wasiojulikana katika mashamba ya chuo hicho hivi karibuni huku chanzo kikikwa bado hakifahamiki. Ibada hiyo imefanyika katika viwanja wa Mochwari ya Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro ambayo imehudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki. Akizungumza mara baada ya ibada hiyo, Dada wa marehemu Liliani Mashuwe amesema mazishi yanatarajia kufanyika katika Kijiji cha Shimbikati kata ya Mkuu, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro Disemba 23, 2021. Anasema wao kama familia wanaziachia mamlaka husika kufuatilia tukio hilo ili kuwabaini waliohusika. Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemble of God (TAG) Dismas Kimario amewataka ndugu wa marehemu kumshukuru Mungu kila jambo kama maandiko ya Biblia takatifu yanavyosema. Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) mkoa wa Morogoro, Ralph Meela alisema kuwa Msi...

Utelekezaji watoto Kilimanjaro, tatizo jipya vita umaskini

Image
Wakati jamii na Serikali wakianzisha juhudi mbalimbali kupambana na umaskini, vijana mkoani Kilimanjaro wanawarudisha nyuma wazazi wao kwa kuwatelekezea watoto wa kulea na kushindwa kufanya shughuli za kujiingizia kipato. Asilimia kubwa ya wananchi waliotembelewa na jopo la wahariri katika wilaya tatu mkoani humo ni wazee wanaolazimika kutunza wajukuu zao, baada ya vijana wao kukimbilia mijini na wengi wao kutofanya lolote kusaidia matunzo ya watoto wao. “Ninaishi na wajukuu tisa,” alisema Donata Lucas Temba mwenye umri wa miaka 53 anayeishi Kata ya Karanga, Moshi Mjini na kuongeza. “Kuna mtoto wangu aliniachia kichanga cha miezi mitatu tu, alikuja kujifungua baada ya miezi mitatu akatoweka.” Mama huyo ana watoto sita ambao baadhi wameshamaliza shule, lakini hawana ajira inayoweza kuwasaidia kuendesha maisha, hivyo kutokuwa na msaada kwa mzazi wao. Licha ya kutokuwa na ajira ya kuaminika, vijana hao wamekuwa wakizalisha au kuzaa na baadaye kuwapeleka watoto kwa bibi yao. ...

Watu wanaongoza kuvunja mahusiano ya kimapenzi

Image
    Katika mahusiano ya mapenzi pamoja na kuwapo kwa sababu mbalimbali zinazochangia mpenzi mengi kufa lakini zipo sababu nyingine ikiwemo watu wanakuzungukua huwa ni chanzo cha kufa kwa mahusiano ya kimapenzi kufa. Wafutao ndiyo watu wanachangia kufa kwa mahusiano;  Wapenzi wa zamani. Hili ni grupu la kwanza la watu wanaovunja mahusiano ya watu wengi na kama sio kuvunja basi kupelekea ugomvi,,usipende kuwa na mawasiliano na ma ex wako hata kama mliachana pasipo na ubaya wowote maana mpenzi wako anapogundua kuwa unawasiliana nae hii inajenga wasiwasi ndani ya moyo wake na wengi hawapendi. Wafanyakazi wenzako.  Hawa nao ni watu unaoweza kuwachukulia kawaida kwasababu tu unafanya nao kazi lakini hawa pia wanachangia,,,utasikia fulani twende lunch,,siku ya kwanza,ya pili,ya tatu mwisho wa siku mnapanga kutoka dinner na mwisho wa siku unamcheat mpenzi wako bila kutegemea. Majirani. Hawa nao ni watu ambao sio wazuri kwasababu ya maneno,,huyu leo atazusha h...

2022 Publisher’s Leading Monetization Format & strategies to your blogs and social media channels

  -This article is very useful for webmasters -In 2022 try to use multtags ads format since it combine all other propeller ads format. -Focus in sport events ie. Africa cup of nations, Olympics, and Fifa world cup contents 2022.  -improve your site SEO and publish the viral contents Read more ➡️ https://propellerads.com/blog/pub-2022-publishers-leading-monetization-formats-strategies #propellerAds #TrafficMonetization #Monetization2022

MTOTO ALIYEFARIKI 2017 NA KUZIKWA AKUTWA AKIWA HAI

Image
  Mtoto mwenye miaka 11 mkazi wa kijiji cha Ngemo kata Ngemo wilaya ya Mbogwe mkoani Geita amezua taharuki kwa kuonekana  hai tena baada ya kufariki miaka  4 iliyopita . Akizungumza na waandishi wa habari  Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishana msaidizi  Henry Mwaibambe amesema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina  Leonard Morisha alifariki tarehe 27 mwezi wa 6 mwaka 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo ,na kushangaza watu kwa kuonekana tena katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama Oktoba  2020 na wazazi wake wakampata na kumtambua Tarehe 12 Desemba mwaka huu.  Katika maelezo yake, Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo alifahamika kwa jina la Tereza Lusolela miaka (48) alithibitisha kuwa kuwa huyo ni mwanaye na baada ya jeshi la polisi kufukua kaburi hakukutwa sanduku wala vipande vya kanga ambavyo mama amedai walimzikia mwanae miaka 4 iliyopita  Sambamba na hilo ACP Henry Mwaibambe ameziomba hospitali kubwa kumsaidia kimatibabu ...

SARUFI YA KISWAHILI NA SINTAKSIA KI311

    MUHTASARI WA SOMO LA SARUFI YA KISWAHILI NA SINTAKSIA  Msimbo wa somo:KI 311  Jina la somo: SARUFI YA KISWAHILI NA SINTAKSIA.  Uzito wa somo: Credit 3  Hadhi ya somo: Lazima  Ufafanuzi wa kozi.  Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia ni kozi inayochambua sarufi ya Kiswahili kwa kuzingatia nadharia za sintaksia kama zilivyoasisiwa na wanazuoni wa isimu. Sintaksia ni tawi la isimu linalohusu namna maneno yanavyounda virai na sentensi za Kiswahili. Sintaksia inahusu tungo za lugha ambazo zaweza kuwa ni maneno, virai, vishazi na sentensi. Japokuwa neno ni kipashio cha kiumbo, linasadifu kuingia katika sintaksia ya lugha kwani lenyewe lina muundo wake unaotokana na viambajengo vinavyoliunda ambavyo ni mzizi na viambishi.  Kozi hii itachunguza nadharia kadha za sintaksia. Awali tutaanza na ubainishaji wa kategoria za maneno tukizingatia umuhimu wake katika sintaksia na muundo wa virai au sentensi. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia za msingi za sint...

Mbinu tatu (3) za kumtongoza msichana ili akubali mapema

Image
  Miongoni mwa maswali ambayo huwachanganya wavulana wengi ni pamoja ni kwa jinsi gani anaweza kumtongoza msichana na hatimaye akakubali. Wengi wao wanakuwa hawana ile nguvu ya kujiamini  ya kumtongoza msichana huyo macho kwa macho, wengi wao utawasikia ooh samahani naomba namba yako. 1. Usimfanye ajue unampenda kwa dhati. Wanaume wengi huwa wanafanyaga kosa hili kubwa . Wanawaambia wanawake wanawapenda au wanahisia za kimapenzi kwao . Ni kweli unampenda , anajua hivyo tayari . Au hajui ? Unampigia simu kila saa , mnataniani kimapenzi na anaona uhusiano wenu kabisa . Kwahiyo japokua anahisi unampenda , usije kuonyesha hivyo kwani anahitaji kusikia kutoka kwako ili ajihakikishia hisia zake . Chukulia poa na usifunguke kuhusu hisia zako kwake , kitendawili alichonacho ndicho kitamfanya azidi kukunata na kutaka kujua mwisho wa mambo . 2. Ishi Maisha mawili Unapoongea nae usiku , mwaga sera zako na funguka kuhusu mambo ya mapenzi sema mkikutana ana kwa ana mch...

Nogesha mahusiano yako ya kimapenzi kwa kufanya mambo haya

Image
    Kutengeneza uhusiano wenye nguvu ni moja ya mambo yenye changamoto kubwa. Japo hakuna maelekezo maalum, kuna mambo machache na rahisi ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako yakaujenga zaidi. Weka desturi ya kusema mambo haya kwa mpenzi wako na muda mfupi tu mtakuwa couple itakayowapa wivu marafiki zetu. Nakupenda Nakupenda ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja. Nilikuwa nakuwaza Ni muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja. Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe. Siku yako ilikuaje? Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu zingine za maisha yake k...

MCHUNGAJI ASHIRIKIANA NA MKE WAKE KUMBAKA BINTI AKAMATWA

Image
  JESHI la Polisi Jimbo la Ogun linasema kuwa limemkamata mchungaji mmoja kwa tuhuma za kula njama na mkewe kumbaka msichana wa miaka 16. Taarifa kutoka kwa kikosi hicho cha polisi nchini Nigeria ilisema Mchungaji Peter Taiwo alikamatwa tangu Ijumaa katika Kanisa la Christ Apostolic Bible Church huko Alaja Oke, Abeokuta. Polisi wanasema mkewe, Elizabeth, pia alikamatwa kwa tuhuma za kula njama ya ubakaji. Aidha, polisi wanasema waliwakamata watuhumiwa hao baada ya msichana huyo kuwalalamikia kuhusu tukio hilo. Msichana huyo alieleza kuwa alipokwenda kanisani katika mazoezi ya kwaya, mke wa mchungaji alimpigia simu na kumwambia aende kwenye chumba ambacho mchungaji huyo alikuwa akimtafuta kwani atampeleka.  Aliingia chumbani na mchungaji akafunga mlango na kutumia nguvu kukidhi mahitaji yake. Alieleza kuwa baada ya mchungaji huyo kumaliza alichokuwa akifanya, mkewe aliingia chumbani humo na kumkuta akilia na kumsihi aache kulia na kumwambia kuwa sasa yeye ni mwanamke huku akimw...

UREMBO WAKUCHA UNAVYOWAWEKA WANAWAKE MATATANI

Image
 Wapo ambao kucha zimeoza, kupata fangasi, kubanduka na kubadilika rangi. Hali hiyo husababishwa na huduma mbovu, bidhaa zisizo na ubora. Pia kushindwa kumudu gharama za huduma za kupaka. Dar es Salaam.  Siyo jambo geni kuona vijana wa kiume wakitembea barabarani hasa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam wakiwa wamebeba vikapu vyenye nyenzo za urembo wa kucha.  Katika vikapu hivyo wanaweka rangi za kucha za aina mbalimbali, vibao vya kusugulia magaga na taulo zikining’inia mabegani ili kuwahudumiwa wateja wao mitaani. Kwa vijana hao ni ajira lakini kwa wanawake ni urembo ili kupata muonekano mzuri wa kucha. Kucha hizo za vidoleni na miguuni husafishwa vizuri kwa maji na kisha kupakwa rangi tofauti kulingana na mahitaji ya muhusika.  Licha ya vijana hao kuzunguka mitaani kusaka wateja, wengine wamejiongeza na kuwa na ofisi maalum ambazo hutoa huduma hizo.  Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumeibuka mijadala hasa katika mitandao ya kijamii kuhusu athari za kiaf...

ALOFONI ZA KISWAHILI PDF

  1.0       UTANGULIZI Alofoni katika lugha ya Kiswahili ni dhana ambayo haijashughulikiwa vizuri. Hii ni kutokana na wataalamu mbalimbali kutofautiana juu ya dhana hii. Tofauti hizi za wataalam zinajitokeza juu sauti za lugha wanazozitoa kama mifano ya alofoni za Kiswahili. Wengine huenda mbali na kusema kuwa lugha ya Kiswahili haina Alofoni. Madhumuni ya makala hii ni kujaribu kuchunguza alofoni katika lugha ya Kiswahili. Na kufikia hitimisho iwapo lugha ya Kiswahili ina Alofoni au la. Na iwapo lugha ya Kiswahili ina alofoni basi alofoni hizo ni zipi? Tutachunguza dhana ya alofoni kama inavyofasiliwa na wataalam mbalimbali, mbinu mbalimbali za kuzitambua alofoni na fonimu za lugha na kisha tutaichunguza mifano mbalimbali ya alofoni inayotolewa na wataalam mbalimbali. Mwisho nitatoa msimamo wangu na kuhitimisha kwa kuchokoza mjadala.   2.0       KIINI Kabla ya kusema Alofoni ni nini kwanza tutoe maana ...