DAKTARI, NESI WASIMAMISHWA KAZI KWA KUFANYA MAPENZI WODINI

Mkuu wa wilaya ya Kaliua, Paul Chacha amewasimaisha kazi watumishi wawili wa hospitali ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kushiriki mapenzi hovyo wodini. Chacha amesema awali ulifanyika uchunguzi baada ya wagonjwa kulalamikia vitendo vya wauguzi hao kufanya mapenzi wodini wakiwa zamu za usiku. Mmoja wa wahudumu hao alikuwa kwenye mafunzo ya vitendo na mwenzake alikuwa ni mtumishi wa hospitali hiyo. Chanzo : CG Fm ====== Siku chache baada ya mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Kaliua, Irene Apina kusimamishwa kazi kwa tuhuma za kukataa kumpa matibabu mtoto wa miaka mitano, wauguzi wawili wa hospitali hiyo wamesimamishwa kazi kwa vitendo vya utovu wa nidhamu. Watumishi hao, mmoja anatuhumiwa kufanya mapenzi wodini na daktari ambaye yupo katika mafunzo kwa vitendo huku mwingine akituhumiwa kuwa kinara katika utoaji wa mimba. Katika kikao chake na watumishi wa sekta ya afya, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua (DC), Paul Chacha aliwasimamisha kazi watumishi hao na kila mmoja kumpa tuhuma zake. DC Chacha...