Baraza la mitihani Tanzania NECTA  limetangaza matokeo ya kuhitimu Darasa la saba hivi leo. Bofya hapa kuona matokeo ya shule zote >>>HAPA>>
Wanafunzi watano wanatokea shule ya Twiboki ya mkoani Mara.

Watano ni wavulana na watano ni wasichana.
Orodha nzima imebebwa na mkoa wa Mara na Dar es Salaam. 

Dar es Salaam. Mikoa ya Dar es Salaam na Mara imeibuka kidedea katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2021 baada ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri kitaifa kutoka katika mikoa hiyo pekee. 
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde akitangaza matokeo hayo leo Oktoba 30, 2021 Jijini Dar es Salaam ametaja orodha ya wanafunzi 10 bora kuwa imetoka katika mikoa hiyo miwili tu.
Dk Msonde akitaja wanafunzi hao amesema nafasi ya 10 kitaifa  imeenda kwa Jackline Manfred kutoka Shule ya Msingi Masaka ya Jijini Dar es Salaam akifuatiwa na Juliana Shimbala wa Shule ya Msingi ya St Joseph ya Dar es Salaam.
Nafasi ya Nane imeenda kwa Rahma Juma kutoka Shule ya Msingi ya Mtuki Highland ya Dar es Salaam huku nafasi ya saba ikienda kwa Barnaba Magoto kutoka Shule ya Msingi ya Twibhoki ya Mkoani Mara.
Joctan Matara kutoka Shule ya Msingi ya Twibhoki ameshika nafasi ya sita na nafasi ya tano imechukuliwa na Eva Chengula kutoka Shule ya Msingi ya Fount of Joy ya Dar es Salaam.
Nafasi ya nne ni yake Joshua Jacob, wa tatu ni John Charles na wa pili ni Happy Deus wote kutoka Twibhoki.
Nafasi ya kwanza imeenda kwa Eluleki Haule kutoka Shule ya Msingi ya St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam. 
Kati ya watahiniwa hao, watahiniwa watano sawa na silimia 50 ya orodha hiyo wanatoka Shule ya Msingi ya Twibhoki ya mkoani Mara. 
Pia katika mchuano huo wa 10 bora kitaifa, ina mgawanyo sawa wa kijinsia ambapo wavulana ni watano na wasichana ni watano. 
Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wengine kwenye masomo sita waliyofanyia mtihani

.