Posts

Showing posts from May, 2021

morogoro; mbaroni kwa kufukua maiti na kunyofoa viungo

Image
  fukua Maiti na Kunyofoa Viungo May 27, 2021 by  Global Publishers Watu watatu wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kufukua mwili wa Rehema Michel, aliyezikwa Jumapili na kutoa viungo mbalimbali ikiwamo kichwa, figo na sehemu za siri.   Mwili wa marehemu Rehema ulizikwa kwenye makaburi ya familia katika Kijiji cha Nguyami, Kata ya Idibo wilayani Gairo mkoani Morogoro.   Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Fotunatus Musilimu alisema tukio hilo lilitokea jana alfajiri katika eneo ambalo ni umbali wa mita 50 kutoka kwenye makazi ya watu kijijini hapo.   Musilimu alisema taarifa za awali zilieleza kwamba mwanamke huyo (35) alipata ajali mjini Morogoro na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na siku chake baadaye alifariki dunia.   Alisema mwili wa mwanamke huyo ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitalini hapo na Mei 23, 2021 (Jumapili) ulisafirishwa na kuzikwa siku hiyo. “Baada ya kumaliza mazishi, leo alfajiri (ju...

Propeller On Air #8: How to champion iGaming Campaign this summer? [live podcast]

  iGaming means the tearms wich cover all form of online gambling whichlst   the term is most commonly associated   with online poker and online casinos. iGaming also extends into sport betting, eSports betting, cryptocurency, binary trading and fantacysports. igaming   campaign in this summer for Advertisers. If you’re a advertiser with sportbetting company is your chance to increase your ROI with propeller ads. Propeller company they accept traffic from igaming site   so if you start to promote your ads it means your ads is showing with many igaming site content and sport streaming site. I hope you will get quality traffic for your business.   For publishers,   igaming industy is now grow higher, many gambler find sport betting tips, many people find for live sportstreaming so if you target this niche your visitors are going to increase times.   Note that now days   there are   many igaming campaign at propeller ads so the CPM ...

publishers absolute guide to traffic monetization

first we suppose to know what is traffic monetization,  in simple way we can say is an act of exchange traffic with revenue  between advertiser and publishers.  for example if your a publisher, social media marketer, content creator, domeiner, or website owner you can get paid for your work by placing certain ads to your  digital  online tools and you will get revenues according to your visitors.  There is different digital ads which publisher can use it to monetize their traffic  and here we speak about best digital ads called propeller ads.  - there are six easy ways to monetize your website with propeller ads ON CLICK  DIRECT LINKS PUSH NOTIFICATIONS IIP, IN PAGE PUSH INTERSTRIALS MULTITAGS  NOTE THAT multi tag is the best ads format since it combine all tag formats Read more here from propeller official site  Article ➡️ https://propellerads.com/blog/pub-publishers-absolute-guide-to-traffic-monetization/ in this link article you ...

Bodi ya Mikopo Kufuta Tozo kwa Wanufaika

Image
  SERIKALI imesema kuwa kuanzia Julai mosi mwaka huu Bodi ya Mikopo (HESLB), itafuta tozo ya asilimia 6 ya kulinda thamani ya fedha inayotozwa kwa wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.   Kauli hiyo imetolewa leo Mei 25, 2021,  Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mhe.  Juma Omary Kipanga  wakati akijibu swali la mbunge wa  Mtambwe Mhe. Khalifa Mohammed Issa  lililohoji ni lini serikali itapeleka Bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria ya mikopo ya elimu ya juu.   “Kuanzia Julai 1, 2021, Bodi ya Mikopo itafuta tozo ya 6% ya kulinda thamani ya fedha inayotozwa kwa wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.   “Vilevile itatekeleza maelekezo yangu ya kuondoa tozo ya asilimia 10 kwa wanufaika wanaochelewa kurejesha mkopo baada ya muda wa miezi 24 kupita baada ya kuhitimu,”  amesema Naibu Waziri Mhe. Kipanga akijibu swali hilo.

sifa majumui za lugha ; taja sifa majumui za lugha

SIFA MAJUMUI ZA LUGHA KATIKA FONOLOJIA Katika sehemu iliyopita tumesema kwamba lengo kuu la fonolojia ni kujaribu kuziweka wazi baadhi ya sifa majumui   zinazojitokeza katika lugha asilia. Maelezo hayo yamejengeka kwenye mantiki kwamba pamoja na ukweli kuwa kunatofauti za wazi   zinazojitokeza   klatika fonolojia ya mifumo mbalimbali ya lugha asilia, bado kuna tofauti fulani ambazo zinaelezwa kuchangiwa lugha zote na lugha zote asilia ndizo zijulikanazo katika taaluma ya fonolojia kama SIFA MAJUMUI ZA LUGHA.   -           KUNA AINA KUU TATU ZA SIFA MAJUMUI ZA LUGHA. Ambazo ni sifa majumui halisi za lugha, sifa majumui pana za lugha, na sifa majumui tabirifu za lugha.   SIFA MAJUMUI   HALISI ZA   LUGHA-   Ni zile sifa za kiisimu ambazo ni zakawaida katika lugha zopte za kibinadamu . mfano katika lugha zote kuna irabu a’ na nikwaidsa katika lugha zote kuwa na utaratibu wa konsonanti na irabu i...

Jinsi ya kukabiliana na mambo yanayozuia wasichana kuwa wabunifu Tanzania

Image
  Ni pamoja na kuondia vikwazo vya kitamaduni na wasichana waanze waamke na kujitoa. Wadau watakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa sahihi kwa wasichana. Pia wametakiwa kutatua changamoto za jamii yao.  Kilimanjaro.  Licha ya juhudi mbalimbali za Serikali na wadau wa maendeleo kuwawezesha wasichana wengi kuingia katika fani ya sayansi, bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowakwamisha kuwa wabunifu.  Changamoto hizo zikiwemo za mifumo na utamaduni zinawazuia wasichana kuonyesha uwezo na kutoa suluhu za teknolojia zitakazosaidia kuboresha maisha ya jamii.  Mei 21 mwaka huu wadau wa ubunifu walikusanyika mkoani Kilimanjaro ili kujadili changamoto zinazokwamisha ubunifu miongoni mwa wasichana na namna ya kuwasaidia kujikwamua na wakatumia ubunifu huo kutoa suluhu zitakazosaidia kuboresha maisha ya jamii.  Mwanzilishi mwenza wa jamii ya wadau wa ubunifu ya Startup Grind Kilimanjaro, Dorcas Mgogwe amesema ubunifu miongoni mwa wasichana upo chini kut...

SELECTION ZA KIDATO CHA TANO 2021/2022

Image
   FORM FIVE SELECTION 2021 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA SITA PAMOJA NAVYUO KWA MWAKA 2021/ 2022  - WALE WOTE WANAOULIZIA MACHAGUO HAYA BADO HAZIJATOLEWA MPAKA LEO MAY 25 LAKINI ZINZWEZA KUTOLEWA MUDA WOWOTE KUANZIA LEO. TEMBELEA MTANDAO HUU MARA KWA MARA ULI UPATE TAARIFA ZAIDI AU TOVUTI RASMI YA TAMISEMI KWA KUBOFYA HAPA www.tamisemi.go.tz

Rostam Feat Ferooz – Hujambo Mwanangu (Official Audio)

Image

Umekata tamaa ya maisha? Tazama filamu hii

Image
Ni filamu ya “Those Who Wish Me Dead” inamuhusu Conor, kijana mwenye umri wa miaka 12 anayepambana ili kufikia ya ndoto ya baba yake. Ni baada ya Baba yake kuuwawa na majambazi ambao wanaendelea kumtafuta Conor ili kufuta ushahidi. Ethan pamoja na mkewe Allison wanaingia matatizoni baada ya kuonekana wao ndiyo wasaidizi pekee wa Conor. Dar es salaam.  Wakati wewe ukiamini katika utendaji wako wa kazi kuwa ni sawa na wa haki, kuna watu wanaona ni kama unawaingilia katika maisha na kazi zao. Wanatafuta jinsi ya kukuondosha ili wao wabaki salama. Hali hii inamkuta Owen, mhasibu mchunguzi ambaye anatafutwa na watu waliosababisha kifo cha bosi wake. Kisa hiki kinapatikana katika filamu ya “Those Who Wish Me Dead” inayopatikana katika jukwaa la Netflix. Ni asubuhi na mapema wanaonekana watu wawili katika nyumba ya muendesha mashtaka wa wilaya. Watu hao wanajitambulisha  kama maafisa wa mamlaka ya gesi na moto na wanapokelewa na mke wa muendesha mashtaka akiwakaribisha ndani na kuwae...

Waziri Mkuu aagiza kutenga Bajeti ya Matengenezo ya Magari 184 ya Maafisa Elimu

Image
  Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmsahauri zote nchini kuhakikisha wanapanga bajeti ya kufanyia matengenezo magari ya Halmashauri ili yaweze kudumu kwa muda mrefu Akizungumza na Maafisa Elimu wa Halmashauri ya zote 184 Nchini wakati wa Uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa  Magari  kwa maafisa  hao yaliyonunuliwa kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo mapema leo katika Viwanja vya Shule ya Sekondari  ya Kibasila  Mkoani Dar-es-salaam amesema ‘Kuna baadhi ya Halmashauri hazitengi bajeti  kwa ajili ya matengenezo ya magari yao , na kusababisha  magari hayo kuharibika mapema na kuwekwa Gereji bila matengenezo  ya Halmashauri zao “Maafisa elimu wa Wilaya Mkikabidhiwa magari haya leo na tukalikuta gari limekaa na halifanyi kazi kwa kukosa matengenezo lazima Wakurugenzi wa Halmashauri watawajibishwa “ amesisitiza Majaliwa Amesema kila Halmashauri lazima iweke mpango wa matengenezo wa magari...

Majina ya wanafunzi kidato chasita waliochaguliwa Jkt

Image
    TAARIFA KWA UMMA WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2021   Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.   Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 hadi 10 June 2021.   Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa, na Makutupora JKT Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.   Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandi...

MCHEPUKO AMUUA MME WA MTU BAADA YA KUNOGEWA PENZI LA MKEWE

Image
  Na Andrew Chatwanga,Songea.  Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Bw. Alfred Nombo (28) kwa kosa la kuumuwa Bw. Erasto Nchimbi (28) mkazi wa Kijiji cha Sara wilayani Mbinga kwa kumchoma na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma Simon Maigwa amewaambia waandishi wa habari leo kuwa tukio hilo limetokea Mei 19 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi. Alisema kuwa Nombo alikuwa na wivu wa kimapenzi kwa mke wa Nchimbi na kuamua kumuua kwa kumchoma na kisu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake. Kamanda Maigwa alisema kuwa Bw. Nombo alinogewa na mapenzi ya mke wa marehemu Nchimbi kiasi cha kupelekea kuvunja ndoa yao  na wivu uliomfanya afanye maamuzi ya kumuuwa mwenye mke ili apate nafasi ya kuwa huru na mke wa Bw. Nchimbi. Aidha Kamanda Maigwa ametoa wito kwa watu wenye uhasama kupeleka matatizo yao katika vyombo vya usuluhishi bad...

Mahakama Kuu ya Tanzania yatupilia mbali wosia wa Dkt. Mengi

Image
     Jaji Mlyambina wa Mahakama Kuu ya Tanzania amesema wosia wa Marehemu Dkt. Reginald Mengi ulioandikwa Agosti 17, 2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia Mahakama imesema, wosia huo ulibagua na kutowaweka katika mirathi baadhi ya watoto bila sababu huku ukiwabakisha Jacqueline Ntuyabaliwe-Mengi na watoto mapacha kuwa ndio warithi Pia, wosia huu unaonesha kuwa, Marehemu Dkt. Reginald Mengi amegawa mali nyingine ambazo si zake pekee yake Mahakama imesema kuwa, wosia huo uliandikwa kipindi ambacho Marehemu Mengi alikuwa hana uwezo wa kuandika wosia kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua tokea mwaka 2016 Aidha, Mahakama Kuu ya Tanzania imewachagua Abdiel Mengi na Benjamin Mengi kuwa Wasimamizi wa Mirathi ya mali alizoacha Dkt. Mengi. Maamuzi haya yameagiza mgawanyo wa mali uanze mara moja

Mwenyekiti wa Mtaa, Madereva Boda Wanusurika Kifo Kisa Dawa ya Nguvu za Kiume

Image
WATU watatu akiwemo Mwenyekiti wa mtaa wa Sanyenge kata ya Old Shinyanga, Benjamin Andrew na waendesha pikipiki wawili wamenusurika kifo baada ya kunyweshwa dawa za miti shamba ‘kienyeji’ na mtu anayedaiwa kuwa mganga wa jadi kutoka nchini Kenya.   Wakizungumzia tukio hilo leo mchana Jumatano Mei 19,2021 baadhi ya ndugu wa wagonjwa hao wamewataja waliopata madhara kutokana na dawa hiyo kuwa ni waendesha pikipiki Benjamin Godson na Peter Bunzari pamoja na Benjamin Andrew ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Sanyenge wote ni wakazi wa kata ya Old Shinyanga.   Wakisimulia kuhusu tukio hilo wamesema kuwa awali ndugu zao walikuwa na afya nzuri lakini baada ya kunyweshwa dawa za kienyeji hali zao zilibadilika wakawa wanatoa udenda na mwili kuishiwa nguvu hali iliyowalazimu wawapeleke kituo cha polisi na kisha Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu.   “Inadaiwa kuwa huyo mganga aliitwa kuja kufichua watu waliovunja duka na kuiba mali. Basi jana mchana wanaume w...

Serikali Kuhakiki Upya Usajili Laini za Simu

Image
  WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amesema huenda wakaanzisha zoezi jipya la uhakiki wa laini za simu zilizosajiliwa kwa alama za vidole lengo likiwa ni kupambana na wahalifu mtandaoni.   Dk Ndugulile ameyasema hayo jana Jumatano Mei 19, 2021 wakati akijibu hoja zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia makadirio ya matumizi na mapato ya wizara yake.   Amesema wanakwenda kuboresha mifumo yao na kwamba Mei 26, 2021 yeye na mawaziri wenzake (hakuwataja) watakaa kuangalia njia bora, wanaweza kubana katika usajili wa simu ikiwa ni hatua ya kupambana na uhalifu huo.   “Tunaweza tukaja na zoezi jipya la uhakiki wa watu waliojisajili kwa alama za vidole ili kuhakikisha wote wenye kadi za simu wamesajiliwa na tunaweza kuweka mifumo ya kuweza kuwabaini,” amesema.   Amesema teknolojia wanayo ya kuangalia jinsi gani ya kuzifungia laini zinazotumika kwenye uhalifu. Kuhusu vizimbuzi kutoonyesha chaneli za Tanzania, Dk Ndugulile amesema am...