Tahadhari: Kimbunga Jobo Kupiga Tanzania

 



KIMBUNGA hafifu kimeyapiga maeneo ya mwambao wa bahari ya Hindi nchini Tanzania jana kufuatia kujitokeza kwa mgandamizo wa hewa katika maeneo hayo.

 

 

 

Kulingana na mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania Kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha ongezeko la upepo hususan katika maeneo ya mwambao wa pwani ya kusini, maeneo ya Lindi na Mtwara.

 

 

 

Samwel Mbuya Meneja wa Kituo kikuu cha utabiri Mamlaka kuu ya hali ya hewa Tanzania amesema kimbunga hicho kipo umbali wa takriban kilomita 930 kutoka pwani ya Lindi na takriban kilomita 1030 pwani ya Mtwara.

 

 

 

Mamlaka ya hali ya hewa nchini imewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia mwelekeo wa upepo na mawimbi ya bahari katika maeneo husika.

 

 

 

Kimbunga hicho pia kilisafiri kwa kasi ya mwendo wa Kilomita 1,022 kaskazini mwa mji mkuu wa Madagascar Antananarivo.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?