Njia thabiti ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) VVU / UKI
VVU/Ukimwi umeenelea kuwa ni moja kati ya changamoto kubwa katika sekta ya Afya duniani haswa kwa nchi zinazoendelea. Kutokana na Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiriwa kuwa, kuna watu milioni 36.9 wanaishi na virusi vya ukimwi duniani kote. Kwa siku za karibuni, kumekuwa na matokeo chanya kwenye mapambano na ugonjwa wa ukimwi, sasa hivi watu wenye virusi vya ukimwi (VVU) wanaishi maisha yenye afya njema na kwa muda mrefu kwa msaada wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (antiretroviral therapy (ART)), pia matumizi sahihi ya dawa hizi husaidia kupunguza muendeleo wa uabukizaji kwa wengine. Kazi kubwa pia imefanyika ili kuzuia na hata kumaliza kabisa maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua. Ingawa kuna matokeo yote hayo chanya, lakini bado kuna sehemu kubwa ya jamii bao haina uelewa juu ya ugonjwa huu, hivyo itakuwa inakuletea dondoo chache juu ya ugonjwa huu; 1. VVU vinaweza kuambukizwa kwa njia mbal...