Wonder Woman 1984”: Filamu ya kufungua mwaka 2020
- Inamhusu Diana ambaye ni mwanadada anayenuwia kuukomboa ulimwengu kutoka kwa watu wabaya.
- Wivu wa Barbara juu ya mafanikio na kunawiri kwa Diana kunamuunganisha na Maxwell kuusumbua ulimwengu.
- Kurudi kwa mpenzi wa Diana, Steve kuna kuwa ni sababu ya Diana kupoteza baadhi ya nguvu zake.
Dar es Salaam. Tuzame kidogo katika ulimwengu wa kufikirika. Diana Prince ni shujaa wa kike ambaye nia yake ni kuukomboa ulimwengu kwa kutumia nguvu zake za maajabu kama mwana Amazon.
Pale anapokutana na Barbara, na kuwa marafiki, urafiki wao hauzai matunda baada ya wivu wa Barbara juu ya mafanikio ya rafiki yake kusababisha kuungana na adui mkuu Maxwell ili apate keki ya mafanikio pale atakapofanikiwa kuuteka ulimwengu.
“Umekuwa ukipata kila kitu wakati watu kama sisi tukiwa hatuna lolote,” anasema mwana dada ambaye wivu wake unamtafuna, Barbara akimwambia Diana.
Maxwell ambaye anatumia satelaiti (Satellite) kufikisha ujumbe wa kuwataka watu kusema kile wanachokihitaji akiwa na nguvu ya kuwafanya wote wavipate kwa kutumia jiwe la maajabu, anamtumia Barbara kama ukuta kati yake na Diana ambaye amenuwia kupambana naye.
Hayo yote yanafanikiwa baada ya Barbara kupata ombi lake la kuwa na nguvu za miujiza kama alizonazo Diana.
Shuhudia kufufuka kwa penzi lililokufa baada ya mpenzi wa Diana kurudi na kumdhoofisha shujaa huyo, kupigana kuisaka haki huku ukijifunza kuridhika na ulichonacho kupitia filamu hii ya “Wonder Woman 1984”
Filamu hii inaonyeshwa katika kumbi za kuangalizia filamu ukiwemo ukumbi wa Mlimani City na Aura Mall kwa Sh10,000 tu. Ni muhimu zaidi katika kipindi hiki cha msimu wa Krismasi na mwaka mpya.
Pia, kama unahitaja filamu ya kumchangamsha mtoto wako, katuni ya ‘The Croods’ sehemu ya pili ni chaguo sahihi kwako
.
Comments
Post a Comment