Siku 16 za kupinga Ukatili Manyara kufanyika Yaeda Chini

 


Manyara

Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia, Mkuu wa kitengo cha Jinsia mkoa wa Manyara  Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Pili Saburi amesema wamepanga kufanya maadhimisho hayo  Yaeda Chini wilayani Mbulu ambapo kumekuwa na vitendo vingi vya kikatili.

Amesema wameamua kuingia zaidi  vijijini ambapo  hapafikiki kirahisi kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo badala ya Mijini palipozoeleka mara nyingi ili nao wapate uelewa na muamko wa kutumia kituo cha polisi kilichofunguliwa katika eneo hilo kuripoti vitendo vya Ukatili.

Ameeleza wanatumia maadhimisho hayo kufikisha elimu kwa jamii, wanafunzi mashuleni, majukwaa mbalimbali, nyumba za ibada na kupitia njia ya redio za kijamii zilizopo mkoani Manyara.

Amesema maadhimisho hayo yamekuwa na matokeo mazuri ambapo wamezidi kupokea wateja wapya ambao wengi wao wanadai walikuwa hawafahamu kwamba vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ni jinai, walikuwa wanadhani ni sawa  Kukeketa, Vipigo ndani ya ndoa wakidhani ni utamaduni.

Wapo watu ambao wameelewa na kuguswa na kueleza kuwa hata vijana watazidi kueneza elimu hiyo kwa wenzao ili waweze kukoma wale wenye tabia ya kufanya  vitendo hivyo vya Ukatili" alisisitiza Pili

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?