MAANA YA UDHANAISHI: UDHANAISHI KATIKA KAZI ZA KIFASIHI, USHAIRI, RIWAYA, TAMTHILIYA
-maana ya UDHANAISHI -misingi au mihimili ya UDHANAISHI -UDHANAISHI katika ushairi -udhanaishi katika riwaya -udhanaishi katika tamthiliya -Udhanaishi ninini pdf DHANA YA UDHANAISHI Katika kuelezea nadharia hii tutajikita kwanza kangalia maana ya udhanaishi kwa mjibu wa wataalam mbalimbali, waasisi wake kisha mihimili yake na mwisho tutamalizia na uchambuzi wa Riwaya ya “Kichwamaji” kwa kutumia nadharia hii. MAANA YA UDHANAISHI Wataalam mbalimbali wameeleza maana ya udhaishi kama vile; Kimani Njogu na Rocha Chimerah (1999) wanasema “Udhanaishi ni nadharia inayojishughulisha zaidi na dhana ya Maisha” swali la kimsingi katika nadharia hii ni ; Maisha ni nini?. Wadhanaishi huchunguza kwa undani nafasi ya mwanadamu ulimwenguni, pia wanajishughulisha na uchunguzi kuhusu uhuisiano uliopo kati ya binadamu na Mungu. Wamitila, K. W. (2003) Katika Kamusi ya fasihi Istilahi na nadharia amefafanua “Udhanaishi ni dhana inayotumiwa kuelezea falsafa ya kuwako na Maisha. Dhana hii...